NAMNA NZURI YA KUPIMA UDONGO.
Ni muhimu sana kufahamu aina ya udongo kabla ya kuanza kilimo cha zao lolote hii itakusaidia kupata mazao bora Zaidi na kwa wingi iwapo pia utunzaji mzuri utazingatiwa.
Maeneo mengi hapa nchini yana udongo tofauti tofauti kulingana na hali ya eneo hilo, kuna maeneo yenye udongo wa kichanga, mengine yana udongo wa tifutifu na mengine yana udongo wa mfinyazi,
Udongo wa kichanga, huu hupitisha maji kwa haraka na mara nyingi hauna rutuba ya kutosha kwa mimea, hupendelewa kwa kilimo cha mazao machache ya mboga mboga iwapo pia utachanganywa na mbolea ya samadi ya kutosha,
Mara nyingi maeneo ya namna hii huwekewa mbolea ya samadi kabla ya msimu wa kupanda kuanza.
Udongo wa tifutifu, huu ni udongo wenye rutuba, mazao mengi hustawi sana kutokana na kuwepo kwa virutubisho vya kutosha, mara nyingi wa kulima wengi hushauriwa kutafuta maeneo yenye udongo wa namna hii, humpatia mkulima faida kubwa bila gharama ya kutumia mbolea nyingi iwapo pia atazingatia huduma nzuri kwenye mazao yake.
Udongo wa mfinyanzi, haupitishi maji kwa haraka na mara nyingi hutuamisha maji, haufai kwa mazao mengi kwa sababu hushikana sana ambapo husababisha kutoruhusu hewa na maji kupita kwenye mmea hivyo huzuia ukuaji wa mmea.
Ili mazao yako yawe na afya bora shambani lazima udongo wako upimwe na udongo mzuri uchaguliwe ili kuweza kufahamu ni virutubisho gani muhimu vinahitajika na kwa kiwango gani.
Udongo lazima uwe na uwiano sahihi wa pH, pH ni kipimo cha alkaline na acid kwenye udongo, uwiano huu husaidia kujulisha kama udongo wako una virutubisho vyote au hauna,
Acid huanzia 0 hadi 6 na alkaline huanzia 8 hadi 14, na 7 ni neutral (uwiano sahihi wa pH kwenye udongo) na ndio unao faa kwa mazao mengi na mara nyingi hufanya vizuri zaidi.
Iwapo udongo wako utakuwa una tindikali ( acid) nyingi Zaidi unaweza kutumia chokaa (lime) ili kushusha kiwango cha tindikali na kuweka uwiano sahihi.
Namna ya kuongeza au kupandisha pH, kiwango cha chokaa (limestone) zinazohitajika kuongeza pH.
kiwango kinachohitajika kuongeza pH kinategemea aina ya udongo uliopo kwenye eneo husika, mfano kwenye eneo la ekari moja ni kama ifuatavyo,
pH kichanga Tifutifu Mfinyanzi
4.0-6.5 1305kg 3175kg 4525kg
Namna ya kushusha pH (alkaline)shambani, kiwango cha sulphur huhitajika kwa kilogram kulingana na ukubwa wa eneo uliopo.
pH Kichanga Tifutifu Mfinyanzi
8.5-6.5 870kg 1175kg 1390kg
Hii husaidia kuweka uwiano sahihi wa pH kwenye shamba lako, wakati mwingine zao sahihi huchaguliwa kupandwa kulingana na pH iliyopo kwenye udongo wako iwapo pH haitawezwa kurekebishwa kwa wakati huo.
NAMNA YA KUCHUKUA SAMPULI
(SAMPLE).
Chukua sample ya udongo kutoka sehemu tofauti tofauti ndani ya shamba lako, kwa kuchimba shimo la urefu wa centimita 20 hadi 25 na hakikisha vyombo vya kuweka sampuli yako ni visafi na vikavu,Baada ya kukusanya sampuli zako zianike juani hadi zikauke vizuri ili ziweze kutoa majibu sahihi, sampuli zenye unyevunyevu mara nyingi hutoa majibu yasiyo sahihi.
![]() |
Jinsi ya kuchukua sampuli. |
Baada ya kuchukua sampuli na kuziweka vizuri peleka maabara ya udongo kwa maandalizi ya kupima
udongo wako ili kujua virutubisho vyote vilivyomo kwenye udongo. baada ya majibu yote kupatikana ripoti huandaliwa ya majibu ikionyesha viwango vyote vilivyopo kwenye udongo. baada ya hapo ushauri unatolewa kulingana na maji ya udongo wako.
![]() |
mfano wa matokeo baada ya kupima udongo |
Veronica J. Joseph
BSc Horticulture
Phone:+255766856431
Email:veronicajj94@gmail.com
0 comments:
Post a comment