UZALISHAJI WA TIKITIMAJI
UZALISHAJI WA TIKITIMAJI
Tikitimaji ni zao la kitropiki linalo tumia siku 65-90 kutoka kupandwa hadi kuvunwa kulingana na aina ya mbegu uliyotumia na hali ya hewa ya eneo husika kwani maeneo ya pwani na yenye joto sana tikitimaji na mazao mengine hukomaa mapema ukilinganisha na maeneo ya milimani yenye baridi kwa hiyo tunashauri kama unataka kulima tikitimaji basi tafuta sehemu zenye hali ya hewa nzuri kuendana na mahitaji yako na soko lako lilivyo
ENEO
Chagua eneo ambalo halina historia ya kuwa na magonjwa au wadudu wanaoshambulia tikiti maji.Eneo ambalo maji yanapatikana kwa urahisi kwa ajili ya umwagiliaji wa tikiti maji ,pia eneo lisilo na udongo wenye chumvi chumvi na unaotuamisha maji soma hapa kujua aina za udongo Namna ya kutambua udongo wenye chumvi na namna ya kuondoa chumvi,Njia za kupima na kutambua aina ya udongo kwenye shamba lako, tikiti maji linastawi sana katika udongo tifutifu na kichanga lakini udongo wa mfinyanzi sio mzuri sana kwa tikiti maji kwani husababisha matunda kuwa na nyufa(cracks)
KUANDA SHAMBA.
Lima shamba lako vizuri kwa kuvunja vunja udongo na pia andaa matuta yenye upana wa mita 2 na urefu kwenda juu sentimita 30 ili kusaidia mizizi ya tikiti kukua vizuri na kuzuia maji kutuaama hasa katika kipindi cha mvua.mfano wa picha kwa uandaaji wa shamba
Nikaribishe kwenye shamba lako nikupe utaalamu namna ya kuandaa shamba kwa ajili ya kilimo hiki na mazao mengine
![]() |
MFANO WA MASHAMBA YALIYOLIMWA VIZURI TAYARI KWA KUPANDA |
MAHITAJI YA TIKITIMAJI
Tikiti linakua vizuri katika udongo unaoshika maji vizuri lakini yasio tuama na kuruhusu mzunguko mzuri wa hewa na maji.Udongo wenye pH 5.8-6.6.pia kama pH ni ndogo tutakushauri cha kufanya ili iweze kuwa nzuri na ya kiasi kwa ajili tikitimaji. Tikiti halistawi vyema ktk baridi na linahitaji joto la udongo kiasi cha 18-29 0c. Joto chini ya 18 0c na juu 29 0c litaathiri kuota kwa mbegu na ukuaji wa mmea.Katika kipindi cha ukuwaji tikitimaji linahitaji unyenyevu wa udongo wakati wote lakini maji yakizidi katika udongo wakati wowote wa ukuwaji na uwekaji wa matunda hupelekea upasukaji wa matunda na kupunguza mavuno na ubora wa matunda.
UPANDAJI
Mbegu/mche wa tikiti maji utapandwa mita 1-2 kati ya mmea na mmea na uwekwa sentimita 2.5 kwenda chini(shimo la kupandia), na kati ya mstari na mstari iwe mita 2,kwa umbali huu panda mbegu 2 kila shimo.Au weka umbali wa sentimita 50 kwa mita 2 lakini hapa panda mbegu moja moja. katika hekari moja utahitaji mbegu gramu 500gms-600gms
![]() |
DOUBLE ROW PLANTING |
![]() |
SINGLE ROW PLANTING |
Mbegu ya tikitimaji utokeza baada ya siku 5-7.
UTUNZAJI WA MMEA.
a) Mbolea.
Mbolea ya samadi kwa kiasi cha 4-6 tani kwa ekari,ichanganye na udongo wiki moja kabla ya kupanda,pia mbolea hii unaweza iweka katika kila shimo siku kadhaa kabla ya kupanda kisha mwagilia ili kupunguza kiasi kikubwa kitakacho hitajika kuweka katika ekari moja.Kama huna samadi tumia Yaramila winner au DAP weka gram 5 kwa kwa kila shimo ,hakikisha mbolea na mbegu havigusani.
Wiki mbili baada ya miche yako kutokeza weka mbolea ya kiwandani -N-P-K (Yaramila winner) gram 5 tena kwa kila shimo,hakikisha unaichimbia chini na isigusane na mmea.
Weka mbolea yenye Calcium kana Yaramila nitrabo gram 10 kwa kila shina unapoona matunda yameanza ili kusaidia kupata matunda makubwa na mazuri.
UMWAGILIAJI
Maji kwa sentimita 1-5 katika udongo yanatakiwa kwa mvua au umwagiliaji ili kupata tikitimaji zuri,kipindi cha muhimu sana kwa mahitaji ya maji kwa tikitimaji ni :kabla ya mche kutokeza ,mwanzo wa kutoa maua na siku 10 za mwisho kabla ya kuvuna.Maji machache kipindi cha kupanda husababisha kutoota kwa mbegu,kipindi cha kuweka maua husababisha matunda machache kutokeza na matunda kukosa maumbo yake.Siku 10 za kuelekea kuvuna husababisha matunda kuwa madogo kama maji ya kutosha yasipopatikana.Matunda yakielekea kuiva punguza umwagiliaji maana kiasi kikubwa cha maji kitasababisha kiasi kidogo cha sukari kutengenezwa na kupasuka kwa matunda, pia kumbuka kweka mfumo wa utoaji maji shambani yaani drainage sytem(nitakuonyesha zaidi nikifika shambani kwako) hii itasaidia kuondoa chumvi na kuhakikisha mazao yanastawi vizuri
Angalizo:
Usimwagilie jion sana hii itasababisha kukua kwa magonjwa kwa sababu ya kuacha majani ya mmea yakiwa na unyevunyevu .Pia angalia wakati mzuri wa uchavushaji /wakati ambao nyuki wanakuwepo shambani mwako hivyo jitahidi kumwagilia mda ambao hautawasumbua nyuki.
Matandazo.
Ni muhimu kutumia matandazo katika shamba lako ili kusaidia kutunza unyevunyevu katika udongo na matandazo haya baadaye yakioza uongeza rutuba katika udongo na pia kusaidia kuzuia kumea kwa magugu na husaidia tunda kutogusana na udongo kitu ambacho kinaweza kusababisha tunda kuathiriwa na joto la udongo au magonjwa kirahisi.Weka matandazo pale mche wako utakapo fikia urefu wa sentimita 10.
Punguza urefu wa mmea
Ili kupata matunda mazuri na yenye afya ni vema kuupunguza mmea kwa mbele ,pale unapoona mmea umefika urefu wa kutosha ili kusaidia kutengeneza matawi ya pembeni ambayo mara nyingi ndio ubeba maua ya kike.
Kuondoa magugu
Ni muhimu sana kuondoa magugu katika shamba lako hasa wiki za mwanzo ili kuzuia ushindani wa mahitaji kati ya magugu na mmea ambapo hupelekea kupungua kwa mavuno na muda mwingine magugu haya yanaweza kuwa ndio chanzo cha baadhi ya magonjwa katika mmea wako
Uchavushaji
Ili kupata kiasi kikubwa cha matunda ni vyema kuwa na mzinga wa nyuki karibu na shamba lako ili kusaidia uchavushaji wa maua ya tikitimaji.Tunashauri uwe na mizinga 1-2 kwa hekari moja.Waweza pia pands alizeti jirani na shamba lako ili kuvuta nyuki.Pia zuia kupulizia dawa za wadudu kipindi cha maua maana unaweza wakimbiza au kuwaua nyuki, kumbuka maua ambayo hayakuchavushwa vizuri huzaa matunda yenye umbo baya lisilo shabihiana na mengine.
Punguza idadi ya matunda
Kwa kawaida tikitimaji uweka zaidi ya matunda manne ,ili kupata matunda makubwa na yenye afya ni vyema kupunguza matunda kwa kuondoa baadhi ya matunda ambayo yanaonekana hayana afya nzuri na yaliopoteza umbo zuri na kuhakikisha kila mche unabaki na matunda 2-3 tu.
Uvunaji
Tikitimaji uvunwa baada ya miezi miwili na nusu hadi mitatu kutoka siku ya kupanda,lakin yapo ambayo hukomaa kwa siku 60-75 kutokana na aina ya mbegu.
Mangonjwa
1) Ubwiru chini (Downy mildew)
Huu ungonjwa husababishwa na fangasi (Pseudoperonosporacubensis).Ni kati ya mangonjwa yanayoshambulia majani na hupendelea sana wakati wa baridi,
Dalili zake:
Majani yaliyoshambuliwa hugeuka rangi na kuwa kama ya njano huku baadhi ya majani yakiwa kama yanakauka na madoadoa meus kwa mbali..
Tiba yake.
Tafuta dawa yenye viambato...Metalaxyl na mancozeb ....kama vile Ridomil gold.
2) Ubwiru juu (Powdery mildew )
Dalili za huu ungonjwa...utaona majani yanakuwa kama yamemwagiwa unga ua majivu
Tiba yake
Tafuta dawa yenye kiambato...Difenoconazole ..kama vile Score.
3) Kata kiuno.(Damping off)
Huu ugonjwa husumbua sana miche midogo,huanzia aridhini ,husababisha miche midogo kuanguka chini baada ya kula sehemu ya shina.
Tiba yake.
Tafuta Ridomil gold na anza kupulizia mara tu baada ya mimea yako kuota.
Wadudu
1) Wadudu mafuta (Aphid)
Hawa hushambulia majani na kufyonza juis ya mmea na baada ya kushambulia majani hujikunja na baadaye kupelekea mangonjwa ya virusi.
Dawa yao.
Tafuta Actara na pulizia majani pamoja na udongo.
Wadudu wengine ni;Nzi weupe (whitefly )-Actara itawamaliza.
,Utitiri mwekundu (Redspidermites)-Dynamec itawamaliza,Thrips-Actara na Dynamec itawamaliza kabisa.
Mbegu bora za tikitimaji.
Kuna mbegu chotara na opv(Sio chotara)
But mbegu bora ni chotara na baadhi ya hizo mbegu ni...
1) Sukari F1-Kutoka East Africa seeds.
2) Sugar king F1-kutoka africasia
3) Juliana F1-kutoka Kiboseed
4) zebra F1-Kutoka Balton.
ambazo zinapatikaana dukani kwetu kwa bei nafuu na ni mbegu bora
SOKO LA TIKITI
Napenda kuwashauri wakulima wetu kuwa njia nzuri ya kulima tikitimaji ni ile ya umwagiliaji, ukiwa mkulima wa tikitimaji lazima uwe mjanja kupanda zao lako ili uje uvune wakati soko liliwa vizuri, mzunguko mzuri wa kupanda tikiti ni huu, panda zao lako katikati ya msimu wa mvua wakati walimaji wa matikiti kwa kutegemea mvua (ambao ni wengi) mazao yao yametoa maua ili wakati wao wanavuna tikiti zao, mazao yako yawe ndio yanaanza kutoa maua kwa hiyo wakati unavuna wakulima wa kutemea mvua watakuwa washamaliza soko lao.Pia kwa wale wanaotegemea mvua ni vizuri uchunguze soko lako vizuri ili uwe na uhakika wa kuuza matunda yako wakati yakiwa tayari yamekomaa.
ukihitaji makala hii kwa mfumo wa Pdf nipigie kwenye number za simu hapo chini
Agronomist Boniphace Mwanje
0719880905
&
ukihitaji makala hii kwa mfumo wa Pdf nipigie kwenye number za simu hapo chini
Agronomist Boniphace Mwanje
0719880905
&
Engineer Octavian Lasway
Irrigation and Water resources Engineer
58 comments:
Do we have watermelon species?
melon spicies zipo za aina mbili tuu ambazo ni water melon and milk melon
milk melon kwa tanzania hatulimi sana lililozoeleka zaid ni water melon
hongera sana mkuuu kwa utaalamu.
asante na karibu uendelee kujifunza zaidi kuhusu uwekezaji kwenye kilimo
Je kati ya tikiti lenye rangi nyeusi na hili la kijani ni lipi lililo bora? yaani linalopendwa zaidi na watumiaji
asante kwa swali lako ....lenye bei nzr na ambalo watu wamelizoea ni lenye rangi nyeusi, lakin yote ni mazuri sema lile hydbrid linakuwa na maji mengi zaidi na mavuna yake ni mengi kuliko hlo lingine
ASANTE SANA BRO NAOMBA NKUTAFUTE PINDI NIKIANZA HYO KAZI
karibu Mr Nicas endelea kusoma makala zetu
Je naweza kupata mbegu au miche ya tikiti maji lenye rangi nyeusi
Nenda kwenye maduka ya kuuza mbegu za tikiti au maduka ya pembejeo , au kwa wakala wa mbegu anaeaminika na ulizia mbegu ya tikiti (local brid)
kaka me ningependa kuulizia gharama na aina za dawa nzuri za kupiga katika kilimo cha matikiti
dawa zinategemea na ugonjwa au wadudu wanao haribu tikiti maji kwa hyo ni vzr mtaalamu auone mmea ulivyoadhirika ndio atakuambia dawa gani inahitajika
karibu
Kama wa watalaam wa kilimo kwann mnasisistiza zaidi ulimaji wa water melon kuliko milk melon kwenye hii ardhi yetu
water melon ni nzr zaid na adaptable kwa hali ya hewa ya kwetu tanzania pia soko lake ni zuri kwani wateja wetu wamezoea water melon kwa hyo katika biashara ya kilimo lazima uangalie mteja wako anataka nini ndio uanze kumtafutia ua kulima kuendana na soko
follow the link below to study more about milk melon and others
http://3.bp.blogspot.com/-mWnV-2lA0Uo/T1cK6Kpv0uI/AAAAAAAAD50/volrei0hTss/s1600/IMG_5360_edited.JPG
Sawa mtaalamu
Je MNA wataaram wa kuweka drip irrigation system shambani?
Mimi ndie mtaalamu wa drip ...karibu sana tuwasiliane 0763347985
Niwapongeze kwa kazi nzuri unayofanya ya kuelimisha jamii juu ya kilimo. Pili nilikua naomba kuuliza kwa mkoa wa pwani ni miezi gani sahihi kwa kulima matikiti?
Asante sana kaka kwa elimu hii ya kilimo cha tikiti maji, vipi unapatikana mkoa gani maana ndo naanza kuandaa shamba ningehitaji zaidi msaada wako hasa wa mbegu maana nimenunua zebra F1 lkn naona kuna bora zaidi.
mtaalamu.!je katika kopo la gram 500 za sukari f1(asali f1) kuna idadi gap.? za mbegu na hutosha kwa ekari gap.?? nataka kujua mtalamu
Nice work! Keep it up broh!
msaada ENG,nataka kujua mzunguko mzuri wa mbolea yaani wakat wa kupanda naweka mbolea gan, na baada ya muda gani tena ninaweka mbolea gan mpaka mavuno???????
Mnatoa elimu nzuri sana kiasi kwamba hata cc tusio na weledi wa kilimo tunaelewa.
Hongera kaka kwa kazi nzuri. Ekari moja ya matikiti inagharimu wastani wa shiling ngap? mpaka uvunaji?
vipi kama eneo lina panya, ntaweza kutumia njia gani, maana wanatoboa sana kabla ya kukomaa vizuri
ASANTE KWA ELIMU ULIOTUPA ENG. LASWAY
JEH!UNAPATIKANA MIKOA IPI KIONGOZI?
500gm kunakuwa na mbegu 5000 ambapo hekari moja inaingia mbegu 4700 endepo utapanda katika spacing ya 60cm kati ya mche na mche na 2m kati ya tuta na tuta
nna robo eka jijini dar es salaam nataka kuanza lima matikiti je ni mbegu gani bora??? na shimo la kupandia mbegu liwe na urefu gani?
Haya ndio mambo ya motherboard Na fatherboard...mh! Hatari!
Mimi pia nataka kufahamu ni miezi gani bora kwa kilimo hiki
Mimi pia nataka kufahamu ni miezi gani bora kwa kilimo hiki
Mimi pia nataka kufahamu ni miezi gani bora kwa kilimo hiki
Mimi nipo Iringa, je hali ya hewa ya huku inafaa kwa tikiti maji
Kwa hekari moja gharama za hichi kilimo ni kiasi gan
Ukiwa nashamba LA heka moja inagharim shingapi kwa kilimo cha tikiti nipo mkuranga pwani
kwakweli nimepata nilichokuwa nakitaka siku nyingi, je kwa ardhi ya misenyi Kagera naweza lima tikitimaji mhandisi?
by Bernard Shija VETA kagera.
Tikt f1 sukar inatakiwa kukata maji kwa muda gani kabla ya kuchuma
Tikiti maji unaacha kumwagilia maji mda gani kabla ya kuvuna
Tikiti unaacha kumwagilia maji mda gani kabla ya kuvuna
Titiki linaachwa kumwagiliwa mda gani kabla kuyatoa
engineer Oct kuinstal drip irrigation system ni shilingi ngapi...tunaomba utuwekee being ya service zenu plz
vp kaka kwa hekali moja drip irrigation inaweza ikaghalim kias gan?
mchanganuo wa gharama kwanzia kuandaa shamba...kununua mbegu mpaka kukamilisha zoezi la upandaji makadirio yake yanaweza yakafikia kiasi gani
i mean per ekari moja kwa kuanzia
Gharama ya kulima eka 1 ni sh ngapi
Asante wataalm kwa kazi ya uekimishaji I really appreciate Pato FI
Asanteni sana wasomaji wetu , tunafurahi kuwahudumia
http://www.greenagricultureskills.com/2017/03/maswali-na-majibu-kuhusu-kitunguu-na.html
pitia hapo tumeweka mchanganuo
Kutokana na wakulima wengi kutaka kujua mchanganuo wa gharama , basi tumeliona hilo na kuwawekea hapa
http://www.greenagricultureskills.com/2017/03/maswali-na-majibu-kuhusu-kitunguu-na.html
Kaka mimi naomba kujua ni mwezi gani mzur kupanda maana nmepata shamba la kulima watermelon mwaka huu shamba lipo karibu na mto luvu
je katika shamba la matikiti maji unaweza ukachanganya na mazao gani mengine?
je unaruhusiwa kuchanganya na zao gani katika shamba la matikiti
safi sana mkuu kwa muongozo
Hongera Mkuu,
kwa masomo unayotupa kila siku,
ubarikiwe sana.
yes nimeelewa vyema
Hongera Mkuu,
kwa masomo unayotupa kila siku,
ubarikiwe sana.
Nimewapata wataalam wet wa kilimo hiki cha tikiti maji .
KUTOKA NA USHAUR WENU KWELI VIJANA LAZIMA TUICHAMKIE HII FURSA MUHIMU KWA KUJIKWAMUA KIMAISHA KUONDOKANA NA UMASKINI TUPO PAMOJA WATAALAM WETU MSICHOKE KUTUFUNZA ZAIDI
Post a comment