FAHAMU NAMNA NZURI YA
KUVUNA MAJI YA MVUA
Eng Octavian Justine Lasway
Irrigation and Water Resources Engineer
Sokoine University of Agriculture
Green Agriculture Company Limited
0763347985/0673000103
Wasiliana na nasi kwa ajili ya usanifu,utengenezaji na ununuzi wa materials
Katika
maeneo mengi ya Afrika mashariki hususani Tanzania tuna kiasi kikubwa sana cha maji kwenye mito, chemichemi,
maziwa na maji ya ardhini(undergroundwater) ambapo asilimia 70% hutumika kwenye
kilimo kwa kuzalisha mazao mbalimbali
Lakini
kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi mvua iliyokuwa
ikitegemewa sana na wakulima kama chanzo cha maji kwa mimea imekuwa sio ya
kuaminika tena kwani hainyeshi tena kwa wakati, hunyesha kwa kiasi kidogo sana(450mm-600mm),
maeneo mengine hunyesha kwa kiasi kikubwa sana mpaka kusababisha mafuriko
ambayo huharibu vibaya mazao ya wakulima mashambani, pia baadhi ya vyanzo vya
maji vimekauka na hivyo kusababisha uhaba mkubwa sana wa maji sio tuu kwenye
kilimo bali hata kwenye upatinaji wa maji safi kwa matumizi ya nyumbani
KWA NINI TUVUNE MAJI YA MVUA
Kama
nilipoeleza hapo awali kuwa kuna baadhi ya maeneo mvua hunyesha kwa kiasi
kidogo sana na hivyo hazitoshelezi kumalizia msimu mzima ili mazao yaliyo
shambani yaweze kukomaa mfano wa maeneo hayo ni Rombo, Same, Lushoto,Baganoyo,kisarawe,mkuranga n.k pia
maeneo ya mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora n.k ambapo mvua inayonyesha katika
maeneo haya inakadiriwa kuwa 550mm kwa mwaka, hali hii imesababisha matatizo
makubwa sana katika maeneo hayo kama kukosekana kwa maji safi, baa la njaa,
kipato kidogo kwa wakulima kwani hutegemea sana kilimo
Kwa
kuliona hilo makala hii itakusaidia kujua namna ya kuvuna maji ya mvua ili
yatumike katika umwagiliaji pale mvua zinapokatika ili kuongeza mavuno kwa
wakulima na waweze kuondokana na umaskini pia utegemezi kwa serikali kwa kutoa
chakula cha msaada
MAMBO YA MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA KUTENGENEZA LAMBO
I.Sura
ya eneo husika(topography and terrain)
Hili ni la muhimu
sana katika kuangalia sehemu ya kutengeneza lambo la kuhifadhi maji ya mvua,
itabidi kuangalia kwa kitaalamu eneo ambalo maji yanatoka ili yaje kwenye lambo
lenyewe(catchment area) pia lazma ifanyike survey ya eneo ambalo lambo
litajegwa ili kuzuia mchanga au udongo kujaza lambo lako inabidi utaalamu wa
kihandisi utumike.
II.Kiasi
cha mvua kinachonyesha katika eneo husika
Hii itakusaidia kujua
na kukadiria kiasi cha maji unachoweza kuvuna pia ukubwa wa lambo kwa ajili ya kutosheleza mahitaji yako
III. Aina
ya udongo
Udongo ni muhimu
zaidi katika kuchagua na kuweza kujua kiasi cha maji kitakacho hifadhiwa katika
lambo lako, pia data za udongo zitamsaidia mtaalamu kukuambia ni zao gani
unatakiwa ulime pia ni kiasi gani cha maji kinachotakiwa wakati wa kumwagilia
ili kupunguza upotevu wa maji na kusaidia mimea kukua vizuri
NAMNA YA KUTENGENEZA LAMBO
Awali ya yote kabla
ya kuanza kutengeneza lambo lenyewe ni kuandaa njia ya kuyakusanya maji(runoff
concentration) kutoka kwenye sehemu mbalimbali kama kwenye mifereji ya
barabara, maeneo ya wazi kama maeneo ya kuegesha magari, maji yanayotoka kwenye
makazi ya watu(rooftop water concentration) kwa hapa unaweza kutumia mawe
(stonebudds) matuta ili kuzuia maji na
kuyaelekeza kwenye mrefeji unaoingia kwenye lambo ila matuta hayo lazima
yapimwe kitaalamu ili yasiharibiwe na maji endapo mvua itakuwu nyingi
Kinachofuata baada ya
hapo ni namna ya kutengeza mfereji unaopeleka maji maji kwenye lambo(grit
channel design and filter drain), kwa kuwa maji yanayokuja huwa na michanga, udongo
au tope ambayo yakiingia kwenye lambo lako husababisha lambo kujaa mapema na
kuhifadhi kiasi kidogo cha maji, kwa hyo sasa mfereji huu inatakiwa uwe na
usanifu mkubwa hasa kwenye mteremko wake(slope) ili kuzuia mchanga,matope na
udongo kuingia kwenye lambo lako
Baada ya hapo lambo linatakiwa lichimbwe kwa ustadi kwa kufuata vipimo husika ili kuweza kuhifadhi kiasi cha maji kinachotakiwa pia kulingana na aina ya udongo katika eneo lako kitaalamu tutakuambia ni aina gani ya material yanayohitajika kwa ajili ya kuweka kwenye lambo lako ili maji yasipotee mfano unaweza kuweka karatasi ngumu za nylon (polythene papers) pia maeneo mengine yanahitaji tuu kushindilia vizuri ardhi ya chini ili iwe imara na isiruhusu maji kuzana chini.
![]() |
Kuzuia matope yasiingie kwenye Lambo |
FAIDA ZA KUVUNA MAJI YA MVUA
a) Kuvuna maji ya mvua inahitaji
gharama ndogo sana lakini maji yanayovunwa ni mengi na huweza kutosheleza
mahitaji ya mimea yako hata kama una shamba la hekari kumi endapo utaalamu
utamika vizuri
b) Maji yanayovunwa humpa mkulima
uhuru wa kuyatumia atakavyo pasipo kubugudhiwa kwa sababu hayana bili wala
malipo unapotumia
c) Maji huvunwa na kutumika mahali
husika kwa hiyo hakuna gharama sana za kuhitaji mabomba ya kusafirishia maji
hayo
Pia
kwa ujumla uvunaji wa maji ya mvua ndio suluhisho pekee la kutatua matatizo ya
maji katika maeneo ammbayo yana uhaba wa maji na yanayokubwa na ukame kwa
kipindi kirefu
Pia
kuna utaalamu mwingine wa uvunaji wa maji ya mvua kwa ajili ya matumizi ya nyumbani
na kwa ajili ya mifugo
Katika
jamii zetu kama utaalamu huu utakuwa endelevu tutasaidika kwa kupata chakula
cha kutosha, kuongoze kipatao na pia kuboresha maisha ya watanzania wengi kwa
ujumla
soma kuhusu kilimo cha vitunguu click hapa,tikiki maji,drip irrigation
Eng Octavian Justine Lasway
Irrigation and Water Resources Engineer
Sokoine University of Agriculture
0763347985/0673000103
4 comments:
Vizuri sana
Thanks a lot mkuu. Elimu hii ni nzuri sana. Labda ungeanisha gharama za mradi huu
Very good and interesting
gharama zinatofautiana sana kutokana na mahitaji
Post a comment