Wednesday, 23 May 2018

UKUAJI WA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KWENYE KILIMO 


Na 
Eng Octavian Lasway 
Irrigation and water resources engineer 
+255763347985/0673000103 
Katika ulimwengu wa sasa ambao maendeleao  na mgeuzi mengi yamefanyika basi kilimo pia kinaendelea kwa kasi hiyo hiyo kama sekta nyingine. Kuanzia zama za mawe, chuma ....n.k tumekuwa tukisoma na kuona namna ambayo mabadiliko ya teknolojia yanavyoathiri biashara na mfumo wa maisha ya watu. Hii yote ni namna ambayo mwanadamu anapambana na mazingira ya kujaribu kuifanya dunia iwe mahali salama Zaidi pa kuishi , lakini pia mabadiliko hayo au namna ya ukuaji wa teknolojia huwa na faida na madhara pia hasa kwenye sekta inayohusu ulaji na afya za watu kama kilimo.

Kuanzia miaka 1990s mabadiliko makubwa yamefanyika kwenye sekta nyingi ikiwepo kilimo kutokana na ukuaji wa matumizi ya kompyuta na mtandao yaani internet  

1. ELIMU 
Kutokana na ongezeko kubwa la mawasiliano na kompyuta sii rahisi mtu yoyote kufanya jambo bila kusoma/ kuingia kwenye mtandao na kuona au kupata elimu juu ya jambo hilo, wakulima wengi wamekuwa waelewa na wasomaji wazuri katika shughuli zao hii elimu husaidia katika kujua mambo mengi Zaidi kama mbegu bora, matumizi sahihi ya madawa na mbegu na kupata uelewa wa shughuli za kila siku katika mashamba yao. 
    Ndio sababu wauzaji na wasambazaji wa pembejeo za kilimo hawataweza kuuza sana kwa kigezo cha punguzo la bei peke yake bali kwa namna ambayo wataweza kuwaelezea na kuwashauri wakulima juu ya ubora na manufaa ya bidhaa husika kwa mfano wakulima wengi watahoji namna ambayo mpando wa msimu huu utaadhiri msimu ujao, athari za kimazingira , afya ya mlaji na uongezaji wa dhamani na mfumo mzima wa mnyororo wa dhamani 

2. Big DATA ( Computer generated information)


katika hili tumeona makampuni makubwa yakiendelea na kupata faida baada ya kuwa chanzo kikubwa cha data , kama ilivyo kupata taarifa ni muhimu sana kabla ya kufanya maamuzi sio tuu ukiwa shamba bali hata mtaalamu au muuzaji katika kumhudumia mkulima , mfano mzuri ni pale unapoenda dukani kununua mbolea ya kukuzia au kupandia mara nyingi muuzaji au mnunuzi humwambia nipe UREA au DAP lakini swali la kujiuliza ni kwamba unapoenda kununua je? kwanini unaweka UREA? je shamba lako lina upungufu wa nitrojeni? au kwa nini unatumia DAP? je shamba lako lina upungufu wa Fosforasi? kama ni ndio kwa kiwango gani? ili ujue kiwango sahihi cha kuweka mbolea lazima uwe/muuzaji awe na data za shamba lako

    Ukuaji wa teknojia katika data umerahisha ufanisi wa biashara na uboreshaji wa mavuno/ mapato kwa wakulima wengi walio endelea zipo teknlojia ambazo husaidia kupata data ili huduma inayotolewa hasa kwenye kilimo ziweze kuendana na mahali, zao, hali ya hewa husika mfano wa Teknolojia hizi ni Agrivi, Farmlog, farmlogic, farmworks, UAV Data na nyingine nyingi.

3. Agriculture Robot 

Kukua kwa teknolojia  lengo lake ni kuhakikisha kazi zinafanywa kwa usahihi na kwa muda mfupi ili kuongeza kipato na mavuno bora, katika hili tunamzungumzia Kijana mmoja Aitwaje Jorge ambae alileta mapinduzi kwenye kilimo na mwaka mwaka 2011 alianzisha kampuni ya Blue River Technology ambao ilianza kufanya utafiti na kuleta mageuzi kwenye kilimo kwa kubuni robot ambazo zimesaidia kupalilia kwa kutumia dawa, kuweka mbolea, kuvuna, kumwagilia na kuweza kuhisi uwepo wa wadudu waharibifu kwenye shamba, na hii ilisababisha kampuni kubwa duniani ya zana za kilimo ya John Deere kuinunua kampuni hii ndogo John Deere robot farming technology

4. Mrejesho wa soko 


Katika hili tumeshughudia mapinduzi makubwa kwenye mifumo ya masoko na hasa uuzaji na usambazaji , hasa kwa kutumia mtandao wa internet (IoT) internet of things 
    Imekuwa rahisi sasa kwa mkulima kujua mlaji anataka nini ili aweze kumzalishia na hii ndio inaweza kufafanua malengo ya mwisho ya uwekezaji mfano mzuri ni wa mitandao ya wakulima wa marekani na ulaya kama Amazon, na nyingine nyingi kwa hapa Tanzania tunayo Ninayo na nyingine nyingi

Zipo teknolojia nyingine nyingi kuendana na mahitaji na mazingira ya watumia kama computerized drip irrigation, Advanced processing machines, genetic engineering (hii husaidia kwenye uzalishaji wa mbegu bora zaidi) 
soma zaidi kuhusu Irrigation technologyHorticulture technologyAgronomy        Reactions:

0 comments:

YouTube

GREEN HOUSE

GREEN HOUSE
BEST DESIGN

Visitors

LIKE US ON FACEBOOK

AGRICULTURE LAND

Mostly Visited