Thursday, 24 August 2017


MATUMIZI BORA YA ARDHI NA MAJI 

KATIKA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

Engineer Octavian J Lasway
Irrigation and water Resources Engineer
+255763347985/673000103

UTANGULIZI 

           Nchi ya Tanzania ni moja kati ya nchi 
yenye ongezeko kubwa la idadi ya watu. Kwa sasa
idadi ya watu inakaridiria kuwa ni milioni 45, na 
tafiti zinaonyesha ifikapo mwaka 2100 idadi hiyo 
itakuwa mara tano ya ilivyo sasa. Katika hili sekta 
ya kilimo ndio miongoni mwa sekta ambazo zinapewa jukumu kubwa la kuhakikisha watu hawa wanapata chakula na mali ghafi  kwa ajili ya viwanda ili kuleta maendeleo na kuinua  uchumi wetu.  Kilimo huajiri takribani asilimia 67% ya watanzania na kukuza uchumi taifa letu kwa ujumla kwani bidhaa za kilimo zinachangia karibia asilimia 30% ya pato la Taifa la Tanzania.(soma zaidi hapa)
Katika Tanzania tumebarikiwa kuwa na eneo la hekta milioni 94.5 kati ya hizo hekta milioni 6.15 ni maeneo ya bahari na maziwa, pia hekta milioni 44 ndizo zinazofaa kwa kilimo na zina udongo mzuri wenye rutuba sawa na asilimia 46.6% ya ardhi yote ya Tanzania ndio rasilimali mama tuliyo nayo sisi watanzania ambapo asilimia 70% ya watu ni wakulima na wanategemea kilimo kama shughuli ya kujipatia kipato na chakula.

Matumizi bora ya ardhi pale ambapo tunaweza kuitumia ardhi yetu kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa za kilimo kwa kuzingatia mbinu za kitaalamu za kuongeza uzalishaji na utunzaji wa mazingira kwani ardhi ikitumika vzuri ni mtaji tosha kwa shughuli za kujipatia kipato , pia matumizi mazuri ya ardhi pasipo kudhuru mazingira husaidia katika kuendeleza uzalishaji kwa muda mrefu kwa kizazi cha sasa na kijacho


Kupima udongo ni muhimu sana kabla ya kuanza shughuli za kilimo kwa udongo ndio hubeba virutubisho ambavyo husaidia mimea katika ukuaji wake na pia udongo ndio unaoleza kwa kina ni zao gani linastawi vizuri katika eneo husika kwa hiyo ili kupata matokeo mazuri ni kufanya kilimo cha kitaalamu zaidi ili kuzalisha bidhaa zenye ubora na kwa wingi ili kuendana na ushindani ulipo kwenye soko la mazao ya kilimo

Maji ndio malighafi ya muhimu katika sekta ya kilimo kwani  katika Tanzania maji ya kilimo ni yale ya Mvua ambayo kwa sasa yamekuwa sio ya kutegemea sana, yapo maji ya mito na maziwa ambayo yanatumika na watu wengi na uwepo wake kwa siku zijazo upo hatarini kwani mito mingi imekauka na mito mikubwa imegeuka kuwa mito ya misimu, chemichemi nyingi zimekauka na nyingine zimepunguza utoaji wa maji kwa asilimia kubwa sana na hii inatokana na mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na shughuli za binadamu ambazo huchangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa vyanzo vya maji na mazingira hasa kilimo holela na ujenzi wa makazi. Kutokana na kupungua kwa maji ya mito na maziwa kimbilio kubwa limekuwa ni maji ya ardhini(underground water). Sasa katika hili la kugeukia maji ya ardhini inabidi kanuni bora na taratibu zifuatwe katika uchimbaji wa visima ili rasilimali hii isije kuadhiriwa kama ilivyotokea kwa upande wa mito na chemichemi. Kuna mifumo mbalimbali ya umwagiliaji, lakini umwagiliaji kwa njia ya matone ndio njia bora zaidi ya umwagiliaji kwani hutumia maji kidogo na ina ufanisi mzuri katika kuhakikisha mimea inapata maji stahiki

UMWAGILIAJI WA MATONE
Ni mfumo wa kisasa kwa umwagiliaji wa mimea na hasa mazao mbalimbali kama tikiti maji, nyanya, papai, vitunguu, karoti, n.k . Katika mfumo huu maji hupelekwa polepole kwa mabomba au mipira yenye matundu madogo moja kwa moja hadi kwenye mmea karibu na mizizi yake. Mfumo huu unaaminika kupunguza sana matumizi ya maji na pia shida nyingine mbalimbali kama zitakavyoainishwa hapa.

HISTORIA YA UMWAGILIAJI WA MATONE
Vyanzo vya mfumo huu vinajulikana kutoka china ya kale ambako wakulima walizika sufuria za kauri katika ardhi karibu na miti na kuzijaza maji. Maji yalipita kwenye kuta za vyombo na kuingia kwenye udongo karibu na mizizi polepole. Wajerumani walitumia mabomba ya udongo wa ufinyanzi uliochomwa ndani ya ardhi kwa umwagiliaji kuanzia karne ya 19. Pia baada ya vita kuu ya piliya dunia mtu wa Australia alianza kutumia mabomba ya plastiki yenye matundu. Ilionekana ya kwamba mbinu hii ni rahisi ina hasara kama mpira ni mrefu, matundu karibu na chanzo cha maji hutoa maji zaidi kuliko matundu ya mbali. Pia kama shinikizo katika mpira ni juu kidogo maji hayatokei kwa umbo la matone bali kwa nguvu mno na kusababisha mmomonyoko wa udongo.
Nchini Tanzania watu walitumia makopo ya maji kwa kutoboa kwenye vifuniko na kugeuza juu chini kisha walichimbia ardhini karibu na shina la mti. Namna hii ilitumika zaidi kwenye kilimo cha miti ya matunda na maua zaidi.
Mfumo wa umwagiliaji kwa matone uliboreshwa nchini Israel na Simcha Bass aliyeongezea nozeli za kutonesha maji. Mpaka hivi sasa Israel ndiyo nchi inayoaminika kwa kutengeneza vifaa mbalimbali vya umwagiliaji kwa matone Pamoja na nchi nyingine kama India, Marekani, Uturuki, China n.k  .
Katika maeneo ya joto kubwa mfumo wote hupelekwa chini ya uso wa ardhi kupunguza tena upotevu kutokana na usimbishaji(Evaporation) wa maji hewani.(Sub surface Irrigation)VITU VYA KUZINGATIA KABLA YA KUANZA UMWAGILIAJI WA MATONE

       1.  Ukubwa wa eneo. Kujua ukubwa wa eneo lako ni muhimu sana ili kujua kiasi cha vifaa vitakavyotosha kwenye hilo eneo lako.
       2. Aina ya udongo.
      Ni muhimu kujua udongo wako kama n kichanga, tifutifu au mfinyanzi hii itamsaidia mkulima na mtaalamu  kujua uwezo wa udongo kuhifadhi kupitisha na kusambaza maji. Kujua hivo kutasaidia katika kupanga kalenda ya umwagiliaji.
 II     3. Sura ya eneo lako ,  hii itasaidia kujua ni namna gani hasa kwenye mwelekeo ya mabomba na mipira ili maji yaweze kufika kila sehemu ya shamba kwa usawa. shamba linaweza kuwa tambarare, mteremko au mwinuko 
I         4. Chanzo cha maji cha uhakika kiwepo. Yanaweza kua maji ya kuvuta toka mtoni au kisimani, maji ya bomba au maji yaliyovunwa na kuhifadhiwa kipindi cha mvua

MFANO WA BWAWA LA KUVUNA MAJI YA MVUA KWA AJILI YA UMWAGILIAJIPia Maji yenye chumvi kiasi hufaa kwa umwagiliaji kwa kutumia drip irrigation kulikonjia nyingine za umwagiliaji.
          5. Aina ya zao. Kila zao lina nafasi yake katika upandaji na kila zao linahitaji maji kwa kiasi chake
DRIP IRRIGATION KWA AJILI YA PASSION FRUITS 
       Kwa hiyo gharama za mfumo huu hutegemea sana na mambo yaliyo elezwa hapo juu

FAIDA ZA UMWAGILIAJI WA MATONE
  a) Matumizi ya maji n kidogo sana ukilinganisha na mifumo mingine ya umwagiliaji. 
   b)Mbolea ya chumvi inaweza kuongezwa katika maji na kufikishwa karibu na miziz moja kwa moja hivyo matumizi yake hupungua kwa kiasi kikubwa.
   c)Maji hupelekwa moja kwa moja pale mimea unapoyahitaji na sio pale yasipohitajika.
   d) Magugu yanapungua kiasi kikubwa shambani isipokua sehemu iliyokaribu sana na mmea.
    e)Hatari ya magonjwa ya fungus inapungua kwa kiasi kikubwa kwasababu majani yanabaki makavu kwa nje.
MFANO WA SHAMBA LA NYANYA , DRIP IRRIGATION HUONGEZA UBORA WA MAZAO


    d)Mfumo unahitaji shinikizo kidogo tu na hii inapunguza gharama za nishati(diesel, umeme) kwa ajili ya pampu.
   f)Hata pampu ikitumika, pampu ni ndogo na rahisi kutumia.
   g) Mmomonyoko wa ardhi hupungua sana shambani kwasababu maji hutoka kwa matone.
    h)Hatari ya kuongezeka kwa chumvi ardhini inapungua sana(magadi).
    i)Mfumo wa matone huongeza mavuno kwa asilimia mia (100%) ukilinganisha na kilimo cha kutegemea mvua. Pia huongeza mavuno kwa 40%-50% ukilinganisha na mifumo mingine ya umwagiliaji.
KITUNGUU HUFANYA VIZURI SANA KWA DRIP IRRIGATION MAVUNO STAHIKI NA UBORA 


MATATIZO YA UMWAGILIAJI KWA MATONE
Zifuatazo ni hasara  zinazoweza kutokea wakati wa umwagiliaji kwa matone
Ø Gharama za mwanzo ni kubwa sana kuliko umwagiliaji wa kawaida hivyo kufanya wakulima wengi kushindwa kufanya umwagiliaji wa matone.
Ø Mipira na vipande vya plastiki vinaweza kuoza na kukatika kutokana na jua.
Ø Kichujio, mipira, mabomba na nozeli katika mfumo zinaweza kuziba kutokana na uchafu mdogomdogo kama haziangaliwi ipasavyo.
Ø Madawa mengi yanayopuliziwa kwenye majani huhitaji maji toka juu/njee yam mea kwa hiyo maji toka kwenye mizizi yanakua hayatoshi kipindi cha madawa.
Ø Mfumo mdogo unaweza kutengenezwa na kila mtu mwenye uwezo kiasi, lakini mifumo kwa shamba zima inahitaji ufundi unaoelewa tabia ya eneo, aina ya udongo, miteremko na miinuko na hali ya maji yanayopatikana.
Ø Mfumo unahitaji kuangaliwa mara kwa mara na mfanyakazi anayeuelewa. Mtu asiyejali anaweza kusababisha hasara kubwa kwa mfano kama bomba linavuja mfululizo matumizi ya maji huwa juu sana.
Ø Panya na wadudu wengine wanaweza kula na kuharibu mipira na mabomba ya plastiki wakitafuta maji.


NINI KIFANYIKE KUKUZA KILIMO KWA NJIA YA MATONE

Ø Kutokana na gharama za kuanza kua kubwa sana taasisi mbalimbali za fedha zisaidie kutoa mikopo kwa wakulima wadogo wadogo kwa kua ni uhakika wakilima kwa kufuata hiki kilimo wataweza kurudisha gharama zote ndani ya mda mfupi
Ø Kutokana na shida ya maji iliyopo wakulima wapewe elimu ya kuvuna maji kipindi cha mvua na kuyahifadhi ili waweze kuyatumia kipindi cha kiangazi kuendlea kulima. Kwa kua mfumo huu huhitaji maji kidogo sana hivyo maji yatakayovunwa yanaweza tosha kwa kilimo.
Ø Wakulima wajitahidi kutumia mfumo huu wa umwagiliaji kwa uangalifu na waweke akiba ya mapato ili waweze kununua vifaa vipya pale mfumo huu unapokua umeharibika na kuharibika kunaweza kua hata kuanzia miaka mpka mitano utunzaji ukiwa mzuri.(Nunua vifaa original)

Wakulima wajitahidi kusoma na kutafuta elimu
zaidi kuhusu teknolojia hasa kwenye kilimo ili 
waweze kuongeza uzalishaji. soma zaidi bofya hapa
Kwa ajili ununuzi wa vifaa, usanifu na ufungaji 
wa Drip Irrigation na aina nyingine za umwagiliaji
wasiliana nasi 

Eng Octavian Lasway 
+255763347985/673000103
info@greenagricultureskills.com 
Reactions:

0 comments:

YouTube

GREEN HOUSE

GREEN HOUSE
BEST DESIGN

Visitors

LIKE US ON FACEBOOK

AGRICULTURE LAND

Mostly Visited