ABDUL MKONO (MWL ABUU)
BSc AEA, SUA
a2mkno@gmail.com
a2mkno@gmail.com
0767359818
0652359818
Eng OCTAVIAN J LASWAY
0763347985/0673000103
MAJIBU:
Kwa zao la kitunguu mnaweza kuanza
kuandaa mashamba mwezi wa tano mwishoni hivi ili mwezi wa sita mwanzoni msie
mbegu kitaluni, ambapo miche itakaa kitalauni mpaka mwezi wa saba katikati au mwishoni,
kisha miche itakwenda shambani wiki ya kwanza ya mwezi wa 8, ambapo utavivuna
mwezi wa 10 katikati. Kisha utavihifadhi mpaka mwezi wa 11 mwishoni/December
mwanzoni utaanza kupata bei nzuri angalau gunia moja la kilo 100-120 utaanza
kupata tsh 100,000-150,000. Mavuno ni gunia kuanzia gunia 70-80 kwa uchache
mpaka gunia 120. Hivyo ujiandae kupata kiasi cha Tshs 7,000,000 mpaka 8,000,000
na zaidi au pungufu pia hii yoote hutokana na matunzo na jinsi ya kuhudumia
shamba Kama ushauri kutoka kwa wataalaumu na kupima udongo. Na hiyo ni bei ya faida kwani kuhusiana na swali lako la kujua gharama
huwa haizidi milioni mbili na nusu (2,500,000) angalia jedwali hapo chini.
Kwa
zao la tikiti maji,
maandalizi ya shamba yanaweza kuanza mwezi wa saba, ili uweze kuzipanda mwezi
wa 8 katikati. Hapa utakuja kuvuna mwezi wa 10. Tikiti hizi za mwezi wa 10
zinabei nzuri sana maana wakati huo ni kiangazi mnoo nchi nzima, kwa hiyo wale
wapambanaji watakaokabiliana na ukame kwa kumwagilia maji, basi mwezi wa kumi
mpaka wa kumi na moja tikiti pia huwa na bei nzuri sana. Lakini pia tikiti za
mwezi wa tatu mpaka wa nne (Wakati wa masika) pia soko lake huwa zuri kwani
kuzalisha kipindi cha mvua kuna changamoto kubwa na wengi hukwama. Huingia miche
2000 mpaka 3000 na ukisimamia vyema unaweza pata matunda 200-3000 yenye kilo
8-12 na kila tikiti kwa bei shambani tsh 1800-2500. Waweza pata 3,600,000 mpaka
7,500,000. Na kwa ekari moja gharama ni kama ths 1,630,000/- hivyo waweza ona
wapata faida nzuri sana ndani ya siku 75. Angalia mchanganuo wa gharama za
tikiti hapo chini katika jedwali
KUMBUKA;
Mavuno
ya mazao yeyote yale hutegemeana na usimamizi uliokuwa bora katika menejimenti
watu, madawa, mbolea na rasilimali pesa kwa ujumla. Kwa kuwa mambo haya
hutofautiana baina ya wakulima katika maandalizi ndio utakuta hata mavuno huja
tofauti pia. Kuhusiana na gharama hapo juu huweza kuongezeka kidogo au kupungua
kutokana na eneo husika, wafanyakazi, au msimu.
0 comments:
Post a comment