Tangawizi ni moja kati ya aina za mazao ya viungo ambayo
sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome). Zao hili kwa lugha ya kigeni
linafahamika kama Zingiber officinale.
UDONGO NA KUSTAWI
Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya kitropiki,
kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1,500 au zaidi. Huhitaji mvua kiasi
cha milimita 1,200-1,800 na joto la wastani wa nyuzi
joto 20°C-25°C. Hustawi vema katika udongo tifutifu wenye
rutuba na usio-tuamisha maji.
AINA
Mpaka hivi sasa hakuna aina rasmi za tangawizi ambazo
zimeainishwa na kuthibitishwa kuzalishwa nchini Tanzania. Pamoja na hili, kuna
aina tatu za tangawizi ambazo zimezoeleka kuzalishwa na wakulima hapa nchini.
Aina hizo ni Tangawizi nyeupe maarufu kama
White Africa au Jamaica, Cochin
(flint), na Bombay.
Tangawizi inayopandwa katika sehemu tambarare huwa laini
zaidi
kuliko inayozalishwa kwenye maeneo ya milima, ambayo huwa
ngumu na kuwa na nyuzi nyingi zaidi.
NAFASI
Nafasi inayotumika kupanda ni kati ya sentimita 23-30 kwa
15-23 na kina cha sentimita 5-10. Unaweza kupanda sehemu yenye
miti au migomba ili kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima
kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji mara
kwa mara endapo mvua inakosekana hadi kufikia mwezi mmoja
kabla ya kuvuna.
MATUMIZI
Tangawizi hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha, harufu
na kuchangamsha katika vinywaji kama vile chai, soda, juisi, vilevi na
kadha-lika. Kuna aina mbalimbali za vyakula ambavyo pia hutengenezwa kwa
kutumia tangawizi kama vile mikate,
biskuti, keki, nyama za kusaga, achari
na kadhalika.
Tangawizi pia hutumika
katika viwanda vinavyotengeneza madawa ya tiba mbalimbali kama dawa za
meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi. Hali kadhalika tangawizi
hutumika katika kutengeneza vipodozi vya aina mbalimbali
vile
kama poda
MBEGU NA NAMNA YA KUPANDA
Zao la tangawizi hupandwa kwa kutumia vipande vya tunguu.
Vipande vya tangawizi huhifadhiwa mahali pakavu penye ubaridi ili kuweza
kuchipua.
Machipukizi hukatwa urefu wa sen-timita 2.5-5. Baada ya
hapo, unaweza kupanda machipukizi hayo kwenye matuta au shambani kawaida endapo
eneo lako ni tambarare.
Baada ya kupanda, tandaza nyasi shambani kuhifadhi
unyevunyevu hasa pale kivuli kinapokosekana.
MATAYARISHO
Ondoa takataka zisizohitajika shambani. Wiki 1-2 kabla ya
kupanda weka mbolea ya samadi au mboji kiasi cha tani 25-30 kwa hekari moja.
PALIZI
Katika kipindi cha wiki mbili, magugu huanza kuchomoza kwa
kuwa udongo huwa na unyevu kwa wingi. Fanya palizi mara majani yanapojitokeza.
Endelea kung’oa magugu na kuweka shamba katika hali ya usafi
hadi wakatiwa kuvuna.
KUPANDA
Tangawizi ni mmea unaotambaa chini ya ardhi, wakati wa
masika hutoa majani juu ya ardhi. Jamaica ina rangi hafifu ya kahawia na tunguu
fupi wakati Cochin ina tunguu fupi zaidi
lenye ngozi ya rangi iliyo kati ya kijivu na nyekundu. Mmea una urefu wa
futimbili na majani yake ni membamba
marefu, ambayo hufa kila mwaka
yakiacha tunguu ardhini likiwa hai. Maua ya mmea huu yana
rangi nyeupe au manjano.
MAGONJWA NA WADUDU
Madoa ya majani:
Yanayosababishwa na viini vya magonjwa viit-
wavyo Colletotrichum zingiberis na Phyllosticta zingiberi.
Kuoza kwa tunguu: Kunasababishwa na viini viitwavyo Pithium
spp.
Mizizi fundo: Inasababishwa na Meloidegyne spp.
UVUNAJI
Tangawizi huweza kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 9-10
baada ya kupanda, wakati majani yake yanapo-geuka rangi kuwa njano na mashina
kusinyaa.
Tangawizi itakayohifad-hiwa ivunwe mapema kabla haijako-maa
kabisa, na ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi na huwa na nyuzi
hivyo hufaa kwa kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana
kulinganana na huduma ya zao, yanaweza kuwa kiasi
cha tani 20-30 cha tangawizi mbichi huweza kupatikana kwa
hekari moja.
SOKO LA TANGAWIZI
Soko la tangawizi lipo ndani na nje ya nchi, kiasi kikubwa
kinauzwa nchini. Bei yake ni kati sh. 300-1,500/- kwa kilo moja kutegemeana na
msimu.
3 comments:
asante sana
ningependa kujua mikoa ambayo ni suitable kwa kilimo cha tangawizi kwa hapa nchini
nabarikiwa na masomo yenu MUNGU awabariki
Je, Tangawizi inaweza kulimwa na ikastawi Arusha?
Post a comment