Sunday, 6 May 2018


VIUMBE WAHARIBIFU KWENYE UFUGAJI WA SAMAKI,MAGONJWA SHAMBULIZI NA HATUA SAHIHI ZA KUDHIBITI (KINGA NA TIBA)Godfrey, Christopher Sway
Mtaalamu wa samaki kutoka 
Chuo Kikuu Cha Kilimo SUA.
+255752799673/0655859810
Wasiliana nasi tukuhudumie katika nyanja zote za ufugaji wa samaki kama vile mpangilio wa mabwawa shambani, utengenezaji wa bwawa, ushauri wa kitaalamu na masoko.     

  UTANGULIZI

Mazingira ya kufugia samaki huwa na vimelea mbalimbali ambavyo huweza kusababisha samaki kupata magonjwa na hatimaye kudumaa au kufa na kusababisha hasara kubwa kwa mfugaji. Hivyo jitihada za makusudi lazima zifanyike kuzuia uwezekano wa kutokea magonjwa na viumbe wengine waharibifu katika mazingira ya ufugaji samaki.
Viumbe wa haribifu kwenye bwawa la samaki si wengi  sana japo kuna malalamiko bado yanayojitokeza toka kwa wafugaji.
Viumbe kama chura, Ndege, Kenge, Kicheche na wengineo wamekuwa wakiripotiwa kuingia marakawamara kwenye mabwawa na kula samaki.
Zifuatazo ni mbinu rahisi za kufanya  ili kuepukana na tatizo hilo;

UDHIBITI WA VIUMBE WA ARDHINI KAMA CHURA  KENGE, NYOKA NA WENGINEO

    Unapotengeneza bwawa lako hakikisha unachimba mfereji wa kina kidogo kwenda chini kuzunguka bwawa lako lote , mfereji huo tandika karatasi ya nailoni ili kuzuia upotevu wa sumu ya ya maji kama unatumia sumu ya maji na kwa anayetumia ya unga kuna haja ya kutandika karatasi hiyo ili kuepusha uharibifu wa mazingira( kemikali zisizohitajika ardhini).  
Umbali toka kwenye bwawa hadi kwenye mfereji angalau  uwe 1m kutoka kwenye bwawa ili kutoruhusu mdudu amakiumbe chochote cha ardhini kuvuka mpaka wako kisha jaza maji yenye sumu ama sumu ya unga.                    

           UDHIBITI WA VIUMBE WA ANGANI HASAHASA NDEGE

 

   Tengeneza  fremu ya miti yenye ukubwa uliozidi bwawa lako kidogo litakaloweza kufunika eneo lote kuzunguka bwawa lako kisha tumia nyavu yenye matundu madogo kama zile zinazotumika kutengeneza madirisha ya nyumba lakini haikikisha matirio yake ni nailoni inayotumika kwenye uvuvi ili kuongezea uimara isioze mapema kisha wamba nyavu hiyo juu ya fremu yako na igongee kwenye kingo za fremu yako ya mabanzi kisha funika juu ya bwawa lako, hii itatumika kama ufuniko mda wote ili kuzuia viumbe wa angani waharibifu kama vile ndege kushindwa kuingia wala kuchukua samaki kwenye bwawa lako wakati wote.

MAGONJWA SHAMBULIZI KWA SAMAKI NA NJIA ZA KUEPUKANA NAYO

      Moja kati ya mifugo isiyoshambuliwa sana na magonjwa ni samaki,lakini pia ni moja kati ya viumbe wanaoweza kuambukizana magonjwa kwa urahisi endapo moja akiathirika na magonjwa na hatua za kumnusuru zisipochukuliwa mapema.
 Malalamiko mengi toka kwa wafugaji ni juu ya fungus,samaki hushambuliwa na fungus hasa kwa samaki wadogo kwa mfano kambale wakati wakuzalisha kwa njia ya kisasa kwa maana utalazimika kuweka mayai  na kuacha vifaranga kwa wiki chache kwenye eneo dogo ili kuwatengenezea mazingira bandia yanayoendana na mazingira asili ili wazaliane(mfano unaweza kufanyia kwenye aquarium yenye kichanja,taa ya joto kwaajili ya kuzaliana),kwa muda huwa mara baada tu ya mayai kuanza kuanguliwa huwa  wanaendelea kula kiini cha yai kwa siku chache za mwanzoni bila kutumia chakula kingine na baadaye atermia kabla ya kuwatoa na kuanza kuwapa chakula cha kawaida,kipindi hiki upo uwezekano mkubwa sana wa fungus kuzaliana kwa wingi na kushambulia samaki kutokana na uwepo wa viini(yolk) na maganda ya mayai ndani ya maji hivyo kupelekea maji kuwa machafu,eneo pia ni dogo,huleta ongezeko la joto,ukiunganisha na uchafu wa taka mwili za samaki hutengeneza mazingira mazuri kwa fungus na bacteria kuzaliana kwa wingi ndani ya maji na kushambulia samaki (mara nyingi huathiri idadi kubwa ya vifaranga wanaoanguliwa kisasa ndani ya aquarium na kuwasababishia vifo maana huambukizana kiurahisi kutokana na maji hutumika kama kisafirishi cha ugonjwa), hili huleta malalamiko mengi toka kwa wafugaji samaki wengi hudai kwanini wakifanya uzalishaji wa kitaalamu kwa kambale huzalisha samaki wengi sana lakini hawakui wote na wengi wanakufa katika hatua hii ya utoto?


     Jibu ni hilo na pia yatupasa kukumbuka kuwa kinga ya mwili dhidi ya magojwa kwa viumbe wadogo ni ndogo haiwezi kulingana na viumbe wakubwa,hivyo inahitajika umakini sana wakuwa karibu na samaki wako hasa wakiwa katika hatua hii ya utoto,zingatia sana usafi wa maji,joto,kiwango cha kemikali ndani(acid na base) na ulishaji,ukiwa makini na hivi hakika utafurahia ukuaji wa samaki wako wote.

Kwa samaki wakubwa vivyohivyo huathiriwa na fungus japo ni kesi chache sana hutokea kwa samaki wakubwa ambazo kwa sehemu kubwa husababishwa na uzembe wa kuto kuzingatia usafi wa maji ndani ya bwawa.


NJIA ZA KUFANYA ILI KUEPUSHA TATIZO HILI

      Hakikisha unabadilisha maji ndani ya wakati maalum,pima usafi wa maji mara kwa mara kwa kutumia search disc ukigundua yameanza kubadilika rangi sana na huioni vizuri ndani ya nusu mita jua maji ni machafu na badilisha.

      Lakini vile vile si uchafu wa maji kwa kuonekana kwa macho tu,pia unatakiwa uwe umejijengea tabia ya kupima hali ya kikemikali ya maji mara kwa mara(yaani kiwango cha acid,base,chumvi,joto)hivi huweza kubadili hali joto ya maji,kuongeza sumu kama ammonia(kutokana na uchafu kama kinyesi toka kwa samaki) na kutengeneza mazingira mazuri kwa vijidudu kama bacteria kuzaliana kwa kasi na magonjwa ya ngozi kama fungus na mengine kuongezeka na  kushambulia samaki wako.

DALILI ZA MAGONJWA YA SAMAKI 

Baathi ya dalili za samaki mgonjwa ni pamoja na kudumaa, kuelea juu juu muda mrefu, kusongamana kwenye chanzo cha maji, kuruka ruka juu ya maji kupita kawaida, kuogelea kwa kasi zaidi na kujigonga gonga kwenye kuta za bwawa, kuwa na vitu vyeupe kama sufi kwenye maji,au sehemu za mwili wa samaki, kuwepo kwa vidoa vyeupe au vyeusi ambavyo si vya kawaida kwenye ngozi ya samaki, kukosa hamu ya kula , samaki kujawa na uteute uliopitiliza juu ya ngozi yake,samaki kukatikakatika baathi ya viungo vyake kama mikia, kuzubaa sehemu moja kwa muda mrefu na vifo.


           JINSI YA KUZUIA MAGONJWA YA SAMAKI

 • Kuchagua sehemu muafaka ya kuweka bwawa kufuatana na ushauri wa kitaalamu
 • kuweka dawa kwenye bwawa ili kuua vimelea vya magonjwa kabla ya kuweka samaki
 • kutumia maji yenye ubora unaotakiwa kwa ajili ya ufugaji wa samaki. Upatikanaji wa maji na ubora wake ni kigezo muhimu katika ufugaji wa samaki
 • Kutumia mbegu bora. Pata vifaranga vya samaki kutoka chanzo kinacoeleweka na kuaminika ambao hukua haraka na kustahimili magonjwa na kumpatia mkulima faida tarajiwa.
 • Usafi wa bwawa. Unashauriwa kufanya usafi bwawani hasa kwa kuondoa majani ili kuepusha wadudu kufanya makazi na hatimaye kuwadhuru samaki.
 • Kuzuia watu, ndege na wanyama wengine kukaribia bwawa. Bwawa lizungushiwe uzio kuzuia watu wasiotakiwa kukaribia bwawa pia hakikisha hamna samaki pori anaeingia bwawani kwani huweza kua chanzo cha vimelea vya magonjwa bwawani.

                  NINI KIFANYIKE BAADA YA KUONA DALILI YA SAMAKI MGONJWA

 • Mtenge haraka samaki uliye muona na dalili hizo ili asiwaambukize  wenzake(mtoe na muweke kwenye bwawa ama chombo cha pekeyake.
 •   Badilisha maji kwenye bwawa hilo na lifanyie usafi wa uhakika bwawa lako,ikiwezekana tumia lime ama dawa nyinginezo salama baada ya kutoa hayo maji na wakati wakufanyia usafi bwawa lako.
 •    Kwa samaki huyo uliemtenga unaweza ukawa unaendelea kumtibia taratibu akiwa katika sehemu tengefu isiyochangamana na wenzake.
 •  Kwa njia nafuu na za kienyeji kama wewe ni mkulima mdogo unaweza tumia maji ya chumvi kama ni magonjwa ya ngozi kwa kumdumbukiza kwa dakika chache kila siku mpaka utakaapoona amepona vizuri.
 •  Usimchanganye na samaki wengine mara tu baada ya kupona,muache kwa muda hata mwezi mzima kwakuwa magonjwa kama fungus yanatabia yakuingia mpaka ndani kwenye damu hivyo yaweza kukudanganya kwa nje kuwa amepona kumbe ndani bado anaugonjwa na kukusababishia hasara ya samakiwako wote.
Godfrey, Christopher Sway
mtaalamu wa samaki kutoka 
Chuo Kikuu Cha Kilimo SUA.
+255752799673/0655859810
Kwa ushauri juu ya utunzaji wa mabwawa, mbegu nzuri ya samaki, chakula cha samaki na namna ya ulishaji wa samaki. 
Reactions:

0 comments:

YouTube

GREEN HOUSE

GREEN HOUSE
BEST DESIGN

Visitors

LIKE US ON FACEBOOK

AGRICULTURE LAND

Mostly Visited