Monday, 7 May 2018

              TARIMO ONIONS PROJECT PLAN- CHEKERENI.


UTAMBULISHO.

Huu ni mpango mkakati au mpango kazi wa Mradi kwa mmiliki wa mradi Mr. Tarimo, mkazi wa Chekereni - Moshi. Kwa kadiri ya Namna tulivyopima udongo katika shamba lako
Mradi huu unasimamiwa kuanzia mwanzo mpaka mwisho na kampuni ya kilimo iliyopo hapa nchini Tanzania yenye makao makuu mkoani Arusha, kwa jina ni Green Agriculture chini ya msimamizi mkuu wa idara ya ufundi wa Vipando na Udongo, Agronomist. Boniphace D. Mwanje, Pamoja na Mtaalamu na Mhandisi wa maji na umwagiliaji Eng Octavian Lasway

DHUMUNI/LENGO LA MRADI.
1. Ni kuhakikisha tunazalisha bidhaa bora na nadhifu.
2. Kuzingatia afya ya mlaji kutokana na bidhaa tutakayo zalisha.
3. Uzalishaji utakaofuata picha halisi ya soko ndani ya nchi au nje ya nchi.

ZAO ELEKEZI.

1. Kitunguu

 
YALIOMO NDANI YA MRADI.

1.Uandaaji wa vitalu pamoja na mashamba.
2.Mbegu elekezi pamoja na upandwaji wake.
3.Mfumo mzima wa mbolea na vipimo vyake.
4.Mfumo mzima wa viatilifu (sumu na madawa) na vipimo vyake.
5.Mfumo mzima wa umwagiliaji kwa zao husika.

1. UANDAAJI WA VITALU PAMOJA NA MASHAMBA.

 KITUNGUU.


Vitalu.

Uandaaji wa vitalu katika zao la Kitunguu halina tofauti kubwa na mazao mengine. Cha kuzingatia ni kwamba hakikisha kitalu chako kinakuwa na upana wa Mita 1 ila urefu unakadiria mwenyewe kulingana na eneo ulilonalo. Kitalu cha Kitunguu hakikisha tuta linakuwa limeinuliwa na liko levo yaani sawa na lisilo ruhusu maji kutuama.
Mashamba.
Uandaaji wa mashamba katika zao la Kitunguu, kwanza ni uaandaji wa visaani (block). Kwa ekari 1 unatakiwa uhakikishe unatoa visahani visivyo pungua idadi ya visahani 200. Tunashauri upana na urefu wa visahani mbalimbali katika shamba la Kitunguu. Kuna visahani vyenye upana wa mita 2.5 na urefu wa mita 5, kuna vyenye upana wa mita 2.5 na urefu wa mita 6 pamoja na vyenye upana wa wa mita 2.5 na urefu wa mita 8. Lakini kwa visahani vya kisasa ni vile vyenye upana wa mita 2.5 na urefu wa mita 6. Pia jinsi ya kuhamisha miche yako penda kuzingatia umbali kati ya mche kwa mche ambao ni kati ya sentimita 3 mpaka 4 pamoja na umbali kati ya mstari na mstari ambao ni kati ya sentimita 6 mpaka 8.
 Kabla ya kuanza maandalizi yote haya kwanza unatakiwa uhakikishe shamba lako liko levo ili ikupe wepesi katika kuweka vipimo vyako.

 MBEGU ELEKEZI PAMOJA NA UPANDWAJI WAKE.

Duniani kuna mbegu za aina mbili, Aina ya kwanza ni mbegu chotara yaani mbegu za kisasa (Hybrid seeds) na aina ya pili ni mbegu za kienyeji au za kukamua (Open Varieties). Lakini sisi kwa mradi wetu huu utaegemea sana katika mbegu za kisasa kwa sababu kilimo chetu ni cha kibiashara kinachohitaji mavuno mengi pamoja na mbegu zisizo shambuliwa sana na magonjwa angali changa.

  KITUNGUU

Mbegu bora katika zao la Kitunguu ni Neptune F1, Jambar F1 pamoja na Rosset F1 kutoka kampuni za Balton na Mosanto katika kitengo cha mbegu. Kwa ekari 1 unatakiwa kuwa na idadi ya mbegu kilo 1.5
Jinsi ya uandaaji wake ni kwamba baada ya uaandaji wa kitalu, utatakiwa uchore mistari yako juu ya kitalu na haitakiwi uchimbe sana kwa maana ukichimba sana kuna uwezekano wa mbegu kuoza au kuchelewa kuota. Utachimba chini waastani wa sentimita 2 mpaka 3 na kati ya mstari na mstari katika kitalu utaacha kati ya sentimita 10 mpaka 15.
Baada ya hapo hauruhusiwi kurudishia udongo wako kwa kutumia kiganja cha mkono na badala yake unashauriwa kutafuta mabanzi ya majani mabichi na kurudishia udongo wako taratibu na kwa kiasi. Kisha utarushia mbolea yako aina ya DAP kwa makadirio juu ya kitalu chako na mbolea tutakazo tumia ni mbolea za Yara, kwa hyo tutatumia Yara DAP kwa zoezi zima la kupandia katika kitalu. Baada ya ya hapo utatafuta majani mabichi na kufunika kitalu chako kisha maji yatafuata kwa juu. Angalizo kifaa kitumikacho kwa umwagiliaji katika hatua hii ya upandaji wa mbegu kitaluni ni keni (Watering Cane). Maji kiasi yanatakiwa yaingie kitaluni na sio maji mengi ambayo yakizidi upelekea kuaribu zoezi la uotaji wa mbegu yako kitaluni.
Katika hatua ya kitalu tutapambana na magojnwa ya ukungu (Kata kiuno pamoja na barafu) pia tutapambana na wadudu wenye sifa ya kufyonza na kutoboa na pia wadudu wenye sifa ya usambazaji wa magonjwa ya virusi  ( Inzi weupe, vimamba, matobozi, vidukari na kadhalika).
Kwa mantiki hiyo, tutatumia dawa aina ya Ridomil Gold kwa kupambana na magonjwa ya ukungu kwa kipimo cha gram 50 kwa maji ya lita 20. Pia tutatumia dawa aina ya Actara au Evisect kwa kupambana na wadudu kwa kipimo cha gram 8 kwa maji ya lita 20.
Mbegu ya Kitunguu inachukua wastani wa siku 10 mpaka 14 kuwa yote imeota katika hatua ya kitalu. Na haitakiwi izidishe siku 35 ambazo ni sawa na mwezi 1 na wiki 1 uwe tayari umesha hamisha kwenda shambani. Laikini kwa ujumla zao la Kitunguu linachukua miezi 4 na nusu mpaka mavuno tangu siku uliyoweka mbegu kitaluni.

MFUMO MZIMA WA MBOLEA NA VIPIMO VYAKE.

Duniani kuna mbolea za aina mbili yaani mbolea za Samadi na mbolea za viwandani. Ila kwa sisi kulingana na maudhui ya mradi tutatumia mbolea za viwandani.
Katika mbolea za viwandani kuna aina mbili (2) za mbolea:-
1. Mbolea za punje
2. Mbolea za majani na maua (Booster).


MBOLEA ZA PUNJE (DAP, NPK, UREA, SA na CAN)


(a) Mbolea aina ya DAP.

Hii ni mbolea ya kupandia. Katika mbolea hii tunalenga kirutubisho kifahamikacho kama Phosphorus (P). Kazi yake kubwa kwenye mmea ulio mchanga ni kuimarisha mizizi na kuifanya iwe na nguvu. Vile vile mmea unavyokuwa mchanga chakula hutengenezwa kwenye mizizi na sio kwenye majani.
Kwenye vitalu vya ekari 1 kwa mazao mengi huwa mara nyingi hutumika wastani wa kilo 8 mpaka 10. Na kwa mkulima anayepanda zao lake moja kwa moja shambani hutumia kiloba kimoja cha kilo 50 kwa ukubwa wa shamba la ekari moja. Kipimo ni gram 5 kwa shimo 1 ambacho ni sawa na kisoda kimoja kwa lugha ya shambani.
Angalizo, hairuhusiwi mbegu na mbolea zigusane. Kwa maana nyepesi ni kwamba hakikisha mara baada ya kuweka mbolea yako rudishia udongo kiasi utakaoweka daraja au ukuta kati ya mbolea na mbegu yako. Kwa kuwa mbolea itaanza udongo utafuata alafu mbegu itafuata na kurudishia udongo wako basi hakikisha chombo ulichowekea udongo mbolea yako kisiwe ndicho chombo utakacho tumia kuwekea mbegu zako. Ikitokea umefanya hivyo mbegu zako zote zitaungua na hazita ota milele. Na ikitokea mtu yule aliyefanya zoezi zima la uwekaji wa mbolea ndiye anayehitajika kupanda mbegu basi lazima ahakikishe ameosha mikono yake na sabuni kabla hajashika mbegu.


(b) Mbolea aina ya NPK.


Hii ni mbolea ya kupandia na kukuzia. Katika mbolea hii tunalenga virutubisho mama vifahamikavyo kama Nitrogen (N), Phosphorus (P) pamoaja na Potassium (K). Kazi zake ni kuhakikisha mmea unaota na kukua.
Kwenye vitalu vya ekari 1 kwa mazao mengi huwa mara nyingi hutumika wastani wa kilo 8 mpaka 10. Na kwa mkulima anayepanda zao lake moja kwa moja shambani hutumia kiloba kimoja cha kilo 50 kwa ukubwa wa shamba la ekari moja. Kipimo ni gram 5 kwa shimo 1 ambacho ni sawa na kisoda kimoja kwa lugha ya shambani. Hii ni mbolea ambayo ukishahamisha zao lako kutoka kitaluni kwenda shambani mara baada ya wiki 1 unatakiwa uweke mbolea hii. Mpishano wake ni kila baada ya siku 21 yaani wiki 3 unatakiwa uweke kulingana na bajeti yako kwa wakati huo.
Angalizo, hairuhusiwi mbegu na mbolea zigusane. Kwa maana nyepesi ni kwamba hakikisha mara baada ya kuweka mbolea yako rudishia udongo kiasi utakaoweka daraja au ukuta kati ya mbolea na mbegu yako. Kwa kuwa mbolea itaanza udongo utafuata alafu mbegu itafuata na kurudishia udongo wako basi hakikisha chombo ulichowekea udongo mbolea yako kisiwe ndicho chombo utakacho tumia kuwekea mbegu zako. Ikitokea umefanya hivyo mbegu zako zote zitaungua na hazita ota milele. Na ikitokea mtu yule aliyefanya zoezi zima la uwekaji wa mbolea ndiye anayehitajika kupanda mbegu basi lazima ahakikishe ameosha mikono yake na sabuni kabla hajashika mbegu.


Mbolea aina ya UREA na SA.


Hizi ni mbolea zinazowekwa kulingana na uhitaji maalum kulingana na asili ya udongo wako kama ni asili ya chumvimchumvi (magadi) au asili ya utindikali.
Mbolea za Urea hizi huwa tunalenga kirutubisho cha Nitrogen tu. Kama shamba lako linatokea kuwa na uhaba wa Nitrogen basi unapaswa kutumia mbolea hii.
Mbolea ya SA (Sulphate of Ammonia), mbolea hii mara nyingi hutumika katika udongo ambao hauna asili ya utindikali. Hutumika kwa mazao kwa kulenga kirutubisho cha Sulphur kwa mmea.
Mara nyingi tunashauri uweke mbolea hii pindi unapoona zao lako limeanza au kukaribia kubeba matunda. Kiwango cha Matumizi ni wastani wa kilo 75 mpaka 100 kwa shamba la ukubwa wa ekari 1. Unaweza kurudia tena kwa mara nyingine kwa utofauti wastani wa siku 21 kulingana na bajeti yako.
Angalizo, hairuhusiwi mche/mmea na mbolea zigusane. Ikitokea umefanya hivyo mimea yako yote itaungua, itakauka na kufa yote.

. (b) Mbolea aina ya CAN.

Mbolea hii ni mbolea tunayolenga kirutubisho mama ambacho ni Calcium (Ca). Kazi kubwa ya Calcium ni kuhakikisha na uimarishaji wa mmea kutoa maua mengi pamoja na kuimarisha hali ugumu wa tunda au zao.
Mara nyingi tunashauri uweke mbolea hii pindi unapoona zao lako limeanza kutoa maua katika hatua za awali. Kiwango cha Matumizi ni wastani wa kilo 75 mpaka 100 kwa shamba la ukubwa wa ekari 1. Unaweza kurudia tena kwa mara nyingine kwa utofauti wastani wa siku 21 kulingana na bajeti yako.
Angalizo, hairuhusiwi mche/mmea na mbolea zigusane. Ikitokea umefanya hivyo mimea yako yote itaungua, itakauka na kufa yote.

MFUMO MZIMA WA VIATILIFU (MADAWA NA SUMU) PAMOJA NA VIPIMO VYAKE.

Duniani tuna viatilifu vya aina nne (4), yaani
1. Chanjo za mbegu (Seeds treatments)
2. Sumu za wadudu (Insecticides)
3. Dawa za magonjwa (Fungicides)
4. Viua magugu (Herbicides).

1. Chanjo za mbegu (Seeds treatments)

Hii ni Chanjo ya mbegu ambayo yenyewe kazi ni kulinda mbegu pindi inapokuwa ardhini iote salama kwa kupambana na wadudu wa ardhini pamoja na magojwa asili ya ukungu katika udongo. Dawa bora ni “Apron star”.
Apron star ni Chanjo yenye viatilifu viwili vya ukungu pamoja na kiatilifu kimoja cha sumu ya wadudu. Kazi yake ni kuhakikisha mbegu yako inaota asilimia 99% labda tu itokee umeuziwa mbegu feki au za kugushi. Apron star ina ujazo wa aina mbili, kuna ujazo wa gram 10 pamoja na ujazo wa Kilo 1 kwa wakulima wakubwa. Ina asili ya poda na ni Nyekundu kwa rangi, ni laini kama unga wa ngano.
Aina ya Matumizi ni kipimo cha pakiti ya gram 10 kwa kilo 4 za mbegu za nafaka. Kwa mkulima wa mazao ya mboga mboga yeye huwa anakadiria kiasi cha msingi ahakikishe kila mbegu imepata dawa. Kwa kuwa ni laini kama ngano basi yakupasa uchanganye mbegu yako sehemu tulivu na isiyo na upepo mkali.


2. Sumu za wadudu (Insecticides).


Hapa tutatumia dawa tofauti kulingana na aina ya mdudu atakaye shambulia shamba au zao.
Actara / Evisect: Hizi ni sumu zinazokabili wadudu wanao toboa na kufyonza pindi mche uko             katika hatua za awali. Wadudu hao pia wanasifa ya kuwa wasambazaji wakuu wa magonjwa ya kupooza, kusinyaa au ukoma mara nyingi hufaamika kama magonjwa ya virusi. Mfano wa wadudu hao ni kama Inzi weupe, Vimamba, Vithiripi, Panzi na kadhalika.
Kipimo cha Matumizi ni gram 8 za Actara kwa Lita 20 za maji.
Baada ya kupiga dawa hii, kwa mazao yote ya mbogamboga hauta ruhusiwa urudie kupiga tena au uvune mara mpaka baada ya siku 14 kupita.
Karate 5 EC/ Match 5EC: Hii ni sumu inayoutumika kuua wadudu wote jamii ya matobozi yaani katapila, Thrips hata vimamba.
Kipimo cha Matumizi: ni 20mls za Karate kwa Lita 20 za maji.
                                         ni 25mls za Match kwa Lita 20 za maji.
Baada ya kupiga dawa ya Karate, kwa mazao yote ya mbogamboga hauta ruhusiwa urudie kupiga tena au uvune mara mpaka baada ya siku 3 kupita.
Baada ya kupiga dawa ya Match, kwa mazao yote ya mbogamboga hauta ruhusiwa urudie kupiga tena au uvune mara mpaka baada ya siku 14 kupita.
Dynamec: Hii ni sumu inayoua wadudu jamii ya chora chora pamoja jamii ya Utitiri. Kwa mfano utitiri mweusi au utitiri mwekundu.
Kipimo cha Matumizi: ni 10 mls za Dynamec kwa Lita 20 za maji.
Baada ya kupiga dawa hii, kwa mazao yote ya mbogamboga hauta ruhusiwa urudie kupiga tena au uvune mara mpaka baada ya siku 14 kupita.
Virtako/ Belt / Collagern: Hii ni sumu inayopambana na wadudu hatari sana kwenye Nyanya anafahamika kama Kantangaze au Boko haramu ila kitaalam tunamuita “Tuta absoluta”
Kipimo cha Matumizi: ni gram 5 za Virtako kwa Lita 20 za maji.
Baada ya kupiga dawa hii, kwa mazao yote ya mbogamboga hauta ruhusiwa urudie kupiga tena au uvune mara mpaka baada ya siku 14 kupita.


3. Dawa za magonjwa (Fungicides).


Hapa tutazungumzia magonjwa sumbufu ya ukungu kwenye mazao yote ya mboga mboga.
Ridomil Gold / Millerz: Hii ni dawa ya ukungu ambayo inazuia na kukinga magonjwa ya ukungu kama kata kiuno pindi mche unavyokua kitaluni, Gonjwa la barafu pamoja na ubwiri unga.
Kipimo cha Matumizi: ni gram 50 za Ridomil gold kwa Lita 20 za maji.
Baada ya kupiga dawa hii, kwa mazao yote ya mbogamboga hauta ruhusiwa urudie kupiga tena au uvune mara mpaka baada ya siku 14 kupita.
Score: Hii ni dawa ya ukungu yenye wigo mpana wa kutibu magonjwa mbalimbali ya ukungu, kama madoa meusi, kutu ya majani, ubwiri unga, barafu. Na mara nyingi pia hutumika hata katika mazao ya miti kama miembe, michungwa, passion na milimao.
Kipimo cha Matumizi: ni 20 mls za Score kwa Lita 20 za maji.
Baada ya kupiga dawa hii, kwa mazao yote ya mbogamboga hauta ruhusiwa urudie kupiga tena au uvune mara mpaka baada ya siku 14 kupita.
Ortiva: Hii ni dawa ya ukungu yenye wigo mpana wa kutibu magonjwa mbalimbali ya ukungu, kama madoa meusi, kutu ya majani, ubwiri unga, barafu. Pia inasifa ya kutunza au kurudisha ujani kibichi wa mmea wako. Hutumika pindi mmea ukishakaribia kukomaa. Na mara nyingi pia hutumika hata katika mazao ya miti kama miembe, michungwa, passion na milimao.
Kipimo cha Matumizi: ni 20 mls za Ortiva kwa Lita 20 za maji.
Baada ya kupiga dawa hii, kwa mazao yote ya mbogamboga hauta ruhusiwa urudie kupiga tena au uvune mara mpaka baada ya siku 3 kupita.

4. Viua magugu (Herbicides).

Kuna aina mbali mbali za viua magugu katika mazao jamii ya mboga mboga. Lakini kulingana na uhalisia wa mradi wetu hatuto tumia na kuzungumzia kilimo hicho.

MFUMO MZIMA WA UMWAGILIAJI  WA ZAO HUSIKA.


Katika mradi wetu tutakuwa na aina mbili za umwagiliaji, yaani umwagiliaji wa matone (Drip irrigation system) pamoja na umwagiliaji wa mifereji (Farrow irrigation system). Mifumo hii yote ni elekezi.Ila sisi kulingana na zao tutahakikisha kila baada ya masaa 72 ambazo ni sawa na siku 3 tunatakiwa kunyeshea maji lakini kulingana na unyevu shambani pamoja na hali ya hewa kwa ujumla amabavyo tumevipata baada ya kupima udongo.
Kadiri mmea utakavyoendelea kukomaa tutakuwa tunaunyima maji kiasi ili tuweze kuruhusu zao likomae vizuri pamoja na kupata idadi kubwa ya mavuno.


KARIBU GREEN AGRICULTURE UFANYE KILIMO CHENYE TIJA

Karibu katika huduma yetu mpya ya FarmCare Kwa wakulima wanaohitaji Wafanyakazi na usimamizi wa mashamba yao 

Engineer Octavian Lasway 
0763347985/0673000103 Reactions:

1 comments:

Unknown said...

Nimejifunza kitu hapo

YouTube

GREEN HOUSE

GREEN HOUSE
BEST DESIGN

Visitors

LIKE US ON FACEBOOK

AGRICULTURE LAND

Mostly Visited