Sunday, 13 May 2018


FAHAMU CHAKULA CHA SAMAKI,UTENGENEZAJI, UHIFADHI WAKE NA ULISHAJI WA SAMAKI.

Godfrey, Christopher Sway
Mtaalamu wa ufugaji wa samaki kutoka
Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo
+255752799673/0655859810        
 Changamoto ya chakula cha samaki hasa kwa wakulima wadogo wadogo hapa Tanzania bado ni tatizo kwani vyakula hivi vina gharama sana. Karibu tukuelekeze fomula nzuri ya kutengeneza chakula cha samaki kwa kutumia malighafi zinazo kuzunguka.     Chakula cha samaki kinachukua asilimia 60-70 ya gharama zote za uzalishaji kuanzia vifaranga hadi kuvuna. Samaki wanatakiwa kulishwa kipindi chote cha uzalishaji wa samaki ambapo kuanzia vifaranga uzalishaji unachukua kuanzia miezi sita hadi nane kufikia mavuno ili kuendana na soko la Tanzania.
    Kuna aina mbalimbali za vyakula vya samaki vinavotengenezwa kwa mchanganyiko wa vitu mbalimbali vyenye virutubisho vyote muhimu vinavyohitajika na samaki husika kulingana na umri wake na aina yake. 

 Mfano : Chakula cha wazazi (brooders) na vifaranga huwa na kiwango kikubwa cha protini ili kuwasaidia wazalishe vifaranga  wengi na ndani ya wakati,lakini pia kusaidia vifaranga waweze kukua kwa haraka na kufikia saizi nzuri ya soko kusudiwa.

Kitaalamu vyakula hivi hutokana na mchanganyiko wa malighafi   kama:


     Mahindi parazwa, dagaa, pumba za mpunga na za mahindi,mtama, pumba za ngano, vitamin mix,madini na vingine vingi mbavyo husagwa na kuchanganywa kwa pamoja kwa viwango maalum kulingana na aina ya  samaki anayeenda kulishwa pia na umri wake.

      Baada ya hapo chakula hiki Kama ni cha samaki wa kubwa ama vifaranga wakubwa kidogo basi kitatengenezwa kuwa katika mfumo wa tambi (pellets) inayoelea na kuanikwa vizuri kwenye kivuli ili kikauke.

     Kama ni cha vifaranga wadogo basi kiache katika mfumo wa poda tu. Kikisha kauka kabisa kihifadhiwe kwenye mifuko maalumu ili kisiharibike.

  NB: Usianike chakula kwenye jua utapoteza virutubisho.MUONGOZO WA MAHITAJI YA VIINILISHE VYA SAMAKI


Wanga 20-25%

Mafuta 10-15%

Vitamin 1-2%

Madini 1-2%

Protini 18-45% 


MALIGHAFI STAHIKI

  • Pumba ya mahindi:  Hii inatumika kam chanzo cha nishati katika ukuaji wa samaki na inachukua mpaka asilimia 25% ya chakula kitakacho tengenezwa. Kiasi utakachotumia kina tegemeana na wingi wa samaki au wingi wa chakula unachokusudia kutengeneza.
  •  Pumba ya ngano au mpunga: Sambamba na pumba za mahindi hizi nazo zinasaidia kama chanzo cha nishati katika ukuaji wa samaki. Sio lazima kutumia zote ila waweza kutumia moja wapo kati ya hizi endapo upatikanaji wake ukiwa ni washida.
  • Dagaa:  Hii ndio malighafi ya kwanza kua na kiasi kikubwa cha protini ambayo ndio inayochangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa samaki hadi kufikia saizi ya soko. Kiini lishe aina ya protini kinachukua asilimia hadi 35% ya chakula chote kinacho tengenezwa kwani ndio kinachochangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa samaki wako. 
  • Malighafi ya soya. Hii ni malighafi inayopatikana kwa urahisi zaidi ukilinganisha na ile ya dagaa. Soya bean inatumika pia kama chanzo cha protini katika ukuaji wa samaki. Kama upatikanaji wa dagaa utakua mgumu unaweza kutumia kiasi kikubwa cha soya bean na kuchanganya kiasi kidogo cha dagaa kulingana na upatikanaji wake.
  •  mashudu ya pamba au alizeti. Mashudu yanakua na kiasi kidogo cha mafuta kwa ajili ya nishati na protini pia kwa ajili ya ukuaji wa samaki.

UHIFADHI WA CHAKULA CHA SAMAKI:


Chakula cha samaki kiwekwe kwenye mifuko maalumu ya kuhifadhia:  
  •   Baada ya kutengeneza chakula hifadhi kwenye vifuko vidogo maalumu
  • Tengeneza kichanja kidogo chenye urefu wa nusu mita na tandika vifuko hivyo  vyenye chakula juu ya kichanja

  • Kichanja kiwe ndani ya chumba chenye kuruhusu mzunguuko wakutosha wa hewa safi ili kuepuka chakula chako kisiharibiwe na bakteria wanaozaliana kwenye joto na unyevunyevu  
  • Kama una chakula kingi sana kichanja chaweza kuwa chenye ghorofa zaidi ya moja au mbili, la msingi ni kuacha nafasi ya kutosha kati ya ghorofa moja na ingine ili kuruhusu hewa yakutosha kupitia 

Njia rahisi ya uhifadhi wa chakula kwa mfugaji mdogo mwenye chakula kidogo:

 

 JINSI YA KULISHA SAMAKI NA MDA SAHIHI WA KULISHA SAMAKI:


Muda sahihi wa kulisha samaki


·  Watu wengi hukosea mda sahihi wa kulisha samaki nahivyo kuathiri afya na ukuaji wa samaki kiujumla.

·   Kitaalamu tunashauri ulishe samaki wako asubuhi kati ya saa tatu kuelekea saa nne na jioni kati ya saa kumi kuelekea saa kumi na moja.

·  Muda huu unapendekezwa kwa sababu joto la maji linakua katika hali nzuri la kumwezesha samaki aweze kula vizuri kwani anakua tayari katika hali ya kuchangamka (active) ukilinganisha na asubuhi sana ambapo maji yanakua na ubaridi mkubwa.

Jinsi ya kulisha samaki;
·   Kitaalamu samaki hupaswi kumlisha kwa makadirio, inatakiwa uchukue sampuli ndogo ya samaki toka kwenye bwawa lako halafu uwapime uzito na urefu, pia ujue ukubwa wa bwawa lako. Hio ndio njia ya kulisha samaki kwa kuzingatia uzito wa miili yao.

·  Kienyeji hasa Kwa wakulima wadogo wadogo, unaweza kukadiria kwa kupima kutumia kiganja chako na kuwatupia kwenye bwawa.

·   Kitaalamu tunashauri kutumia eneo moja tu la kuwalishia samaki wako kila siku, kama umeamua kuchagua kona moja ya bwawa hakikisha unatumia hiyo kila siku.
 Wasiliana nasi kufahamu zaidi namna ya kutengeneza chakula cha samaki, Ulishaji na Uhifadhi wake
Godfrey, Christopher Sway
mtaalamu wa samaki kutoka
Chuo Kikuu cha Kilimo SUA
+255752799673/0655859810

 

Reactions:

0 comments:

YouTube

GREENAGRICULTURE APP

GREENAGRICULTURE APP
GREENAGRIC APP

visitors

LIKE US ON FACEBOOK

AGRICULTURE LAND

Mostly Visited

GREEN APP