ONGEZA KIPATO CHAKO MARADUFU KWA KUFUGA SAMAKI AINA YA PEREGE KIBIASHARA
Godfrey, Christopher Sway
Mtaalamu wa samaki kutoka
Sokoine University of Agriculture
+255752799673 / 0655859810
Ufugaji samaki ni kazi ya kupanda, kukuza na kutunza samaki katika mabwawa, mito, mifereji au eneo lililotengwa kwa ajili ya ukusanyaji wa maji, (water harvesting ponds) uzio (uliotengenezwa kwa vyuma, nyavu au miti) au eneo lolote ambalo udhibiti wake yako chini ya mamlaka ya mfugaji mwenyewe. Mabwawa ya samaki hutengenezwa au huchimbwa kwa njia tofauti tofauti, yaweza kuwa ni ya kuchimbwa na watu (japokuwa ya asili pia huweza kutumika) Samaki pia wanaweza kufugwa baharini au ziwani kwa kutumia vizimba (cages) Pia uzio unaweza kuwekwa katika eneo lolote lililo na maji kama ziwa au baharà au chemichemi. Perege /sato /Tilapia wapo wa aina tofauti tofauti kama vile perege wa Mosambique, Perege weusi, perege wa victoria na wale shiranus. Tofauti zao ni ndogo sana na mara nyingi ni vigumu kuwatambua.

Ufugaji samaki kwa kiasi fulani si sawa na ukuaji samaki katika mito, maziwa na bahari. Tofauti iko katika huduma inayotolewa kwa samaki wafugwao na idadi ya samaki wanaopaswa kuwamo ndani ya eneo husika. Samaki waliofugwa huhitaji kulishwa na kuhudumiwa.Ufugaji wa samaki ni sector inayokua kwa kiasi fulani licha ya changamoto zinazo ikabithi sector hii hapa Tanzania. Baadhi ya Watanzania wamekuwa wakifuga samaki katika mabwawa
hata kabla ya nchi yetu kupata uhuru. Lakini baadhi ya wafugaji wamekuwa wakitoa matunzo hafifu kwa kutofahamu vizuri mambo ya kuzingatia katika swala zima la ufugaji wa samaki kiasi cha kufanya mavuno kutokua mazuri na kupelekea sector hii kushuka na kukua kwa kusua sua. Kwa miaka ya karibuni, serikali imetilia mkazo utoaji elimu (ugani) wa ufugaji samaki ili
kuboresha mafanikio yake. Wasomaji wetu wa makala hii watasaidika kuogeza uelewa zaidi kwenye ufugaji wa samaki.
MWONEKANO WA PEREGE / SATO NA UMBILE LAKE
Faida za ufugaji samaki
Hizi ni baathi ya faida za ufugaji wa samaki (perege)
1. Chakula bora chenye uto-mwili
(protini) muhimu inayohitajika kujenga mwili.
2. Kujipatia kipato baada ya
kuuza samaki waliofugwa.
3. Kuboresha kazi nyingine za
kilimo kama bustani ya mboga, ufugaji wa ng’ombe, bata, kuku, nguruwe, bustani
ya miti, n.k.
4. Huwezesha kutumia rasilimali
ambayo isingekuwa ikitumika kama kusingekuwa na ufugaji samaki kama vile
eneo la ardhi lenye maji maji, pumba za mahindi na mpunga, na mabaki ya mboga mboga
kutoka bustanini kwa kulishia samaki.
5. Eneo la bwawa huwa ni sehemu
nzuri ya mapumziko.
6. Perege pia wanasoko kubwa hapa
Tanzania kwan wanakubalika na watu wote.
Hatua muhimu kuzingatia katika shughuli za ufugaji samaki
1. Uchaguzi wa
mahala panapofaa kwa ajili ya kuchimba bwawa la samaki.
2. Tathmini ya
umbo na ukubwa wa bwawa
3. Uchimbaji wa bwawa.
4. Uingizaji na utoaji wa maji
katika bwawa.
5. Uwekaji wa mbolea na (majivu).
6. Upandaji wa vifaranga vya samaki.
7. Ulishaji wa samaki na matunzo
mengine bwawani.
8. Uvunaji wa
samaki na aina ya nyavu/zana zifaazo kutumika.
9. Uhifadhi wa
mbegu kwa ajili ya mzungoko mwingine wa upandaji samaki bwawani.
Vigezo muhimu katika kuboresha uzalishaji
Joto au ubaridi wa maji katika sehemu husika huweza kuongeza au kupunguza hamu ya ulaji wa samaki na hivyo ukuaji wake.- Chakula cha samaki (cha asili na cha ziada), aina ya chakula na kiasi kinachopatikana. Chakula cha asili ni kama vile planktonik au majani na algae wanaoota kwenye mabwawa.
- Uwingi wa samaki waliomo bwawani kulinganisha na ukubwa wa bwawa. Hapa lazima wingi wa samaki uendane na ukubwa wa bwawa lenyewe.
- Ubora wa vifaranga (quality) waliopandwa. Vifaranga wenye ubora mzuri huwa na uwezo wa kukua haraka.Na hapa pia mkulima anaweza kuamua kuchagua mbegu nzuri za jinsia moja (mono sex) au mchanganykio wa jinsia kwa ajili ya kupata mbegu za mzunguko mwingine.
Wasiliana nasi kwa ushauri, utengenezaji mabwawa, upatikanaji wa mbegu bora, utengenezaji wa chakula cha samaki, ulishaji wa samaki, na Eneo linalofaa kwa ufugaji wa samaki.
Godfrey, Christopher sway
Mtaalamu wa samaki kutoka
Chuo kikuu cha SUA Morogoro
+255752799673/ 0655859810.
0 comments:
Post a comment