Tuesday, 24 April 2018

Uchaguzi wa aina gani ya samaki inayofaa kufugwa bado inaonekana kuwa ni changamoto hasa kwa wakulima wadogo wadogo hapa nchini kwetu. 

Godfrey, Christopher Sway
Mtaalamu wa samaki kutoka
Sokoine University of Agriculture
+255752799673/0655859810.
Kwa mahitaji ya ushauri, Utengenezaji na Utunzaji wa mabwawa ya samaki wasiliana nasi


 Kitaalamu haishauriwi uchague aina yoyote ya samaki kutokana na mapendeleo binafsi,uchaguzi wa aina gani ya samaki anapaswa afugwe katika mazingira gani utafanyika mara baada ya kuchukua vipimo maalum vya kitaalamu katika eneo husika.
Vipimo hivyo ni kama vile Kiwango cha chumvi,Kiwango cha hali joto ya maji na eneo husika kiwango cha asidi au bezi (PH) ambayo hupimwa kwenye udongo wa eneo husika na maji ya eneo husika na kulinganishwa na zile ambazo samaki wa aina hiyo huweza kuhimili na ndipo utakapo weza kuchagua ni aina gani ya samaki ufuge.
Kwa maeneo mengi yaliyopo nchini kwetu samaki kama sato(Tilapia niloticus,tilapia moossambicus,Cat fish (Clarius species) hawa kwa upande wa maji baridi wameonekana kufanya vizuri zaidi.
  Mfano: Tilapia anafanya vizuri kwenye hali joto kati ya 20 C-28 C, na pia hufanya vizuri kwenye Ph kati ya 7-8.
Kwa upande wa samaki wa maji chumvi kwa Tanzania samaki kama Prons, Robusta, Milkfish na wengine wengi wanafanya vizuri japokuwa ufugaji huu wa maji chumvi ni mrahisi kufanyika kwenye madema(cage), Race ways(vizuizi), pia ni rahisi kwa kutumia mabwawa ila tu ni kwa wafugaji walioko karibu na bahari

 Sato/Tilapia

Perege /sato /Tilapia wapo wa aina tofauti tofauti kama vile perege wa Mosambique, Perege weusi, perege wa victoria na wale shiranus. Tofauti zao ni ndogo sana na mara nyingi ni vigumu kuwatambua.
Ufugaji samaki kwa kiasi fulani si sawa na ukuaji samaki katika mito, maziwa na bahari. Tofauti iko katika huduma inayotolewa kwa samaki wafugwao na idadi ya samaki wanaopaswa kuwamo ndani ya eneo husika. Samaki waliofugwa huhitaji kulishwa na kuhudumiwa.    
         

Kambale/Catfish:

 Kambale (Claries gariepinus), ni aina ya samaki ambao wanafugwa kwenye maji baridi na wanauwezo wa kustahimili mazingira magumu kulinganisha na samaki wengine.Samaki hawa wapo spicies au wanatajwa kwa majina mbalimbali kulingana na eneo na jamii husika. Samaki hawa unaweza kusikia wakitajwa kwa majina mengine kama vile, kambale channel, koleo, samaki kidevu, samaki wa kwenye matope. N.k. Samaki hawa (kambale) wanakua kwa kiasi kikubwa sana kwanzia kilo 3 na kuendelea.Kambale hawana magamba na wanauwezo wa kustahimili upungufu mkubwa wa oxygen kwenye maji ya bwawa kwakua na mifumo miwili ya upumuaji katika mwili wao.Zingatia haya kwa baadhi ya aina ya samaki wanaofugwa zaidi hapa Tanzania

   Kwa samaki aina ya Tilapia niloticus na tilapia Mossambicus hawa wanatabia ya kuzaliana sana ndani ya mda mfupi pia usipokuwa makini kuthibiti wingi wao kulingana na ukubwa wa bwawa na chakula unachowapatia inaweza kuwaathiri sana katika ukuaji wao na kuwasababishia kudumaa, jambo ambalo huwasumbua sana wakulima wengi hulalamika swala la kudumaa kwa samaki.

JINSI YA KUEPUKANA NA TATIZO LA SAMAKI KUWA WENGI BWAWANI


 Kwanza hakikisha idadi ya samaki waliopo kwenye bwawa lako inaendane na uwezo wa bwawa hilo kuhimili ujazo  huo (kwa kila 1m² wanatakiwa wawe samaki 4-5, hivyo chukua na ukubwa  wa bwawa  lako halafu fanya mahesabu utajua wawe wangapi kwenye bwawa hilo).

 Pia chakula unachowapatia hakikisha kinawatosha na pia unalisha chakula chenye virutubisho husika kulingana na aina husika ya samaki (kama ni mtoto au mzazi basi wapatie chakula chenye protini ya kutosha ili wakue vizuri na kuzaliana).
     Pia unatakiwa uepuke tatizo la kupishana kwa ukuaji wa samaki ndani ya bwawa kwa kuwatenganisha kulingana na ukubwa wa miili yao (gredding and sorting).
     Zoezi hili unalifanya kwa kutumia nyavu maalumu zenye matundu yenye ukubwa tofauti kwa kutumia njia yauvunaji kwa kila nyavu, wakati huo  uwe umeandaa beseni ama vyombo vya kutosha kuweka humo kulingana na ukubwa wao kwa kila chombo.

Baada ya hapo hakikisha kila samaki walioko katika kila chombo unawaweka kwenye bwawa tofauti na wengine ili kudumisha uwepo wa uwiano mmoja katika ukuaji wao.

MADHARA YA KUCHANGANYA SAIZI TOFAUTI NDANI YA BWAWA MOJA.

    Canibalism(kulana wenyewe kwa wenyewe) hii hutoke sana hasa kwa samaki aina ya kambale hawa wakitofautiana ukuaji huwa wale wakubwa huwala wadogo na baadae huadhiri jumla ya mavuno yako.
 
Ugombaniaji wa chakula, maji, eneo,hewa, na ongezeko kubwa la joto hivi huathiri ukuaji wa samaki na kuwafanya wadumae, wafe hasa kwa wale wanyonge na wadogo.

 Kwa mahitaji ya ushauri, utengenezaji na utunzaji wa mabwawa ya samaki, wasiliana nasi:
Godfrey, Christopher Sway
mtaalamu wa samaki kutoka
Chuo kikuu cha Kilimo SUA.
+255752799673/0655859810.

Reactions:

0 comments:

YouTube

GREEN HOUSE

GREEN HOUSE
BEST DESIGN

Visitors

LIKE US ON FACEBOOK

AGRICULTURE LAND

Mostly Visited