Saturday, 31 March 2018


PATA MATOKEO MAZURI KWA KUFUGA SAMAKI AINA YA KAMBALE KWA KUZINGATIA USHAURI WA KITAALAM

 Godfrey, Christopher Sway
 Mtaalamu wa Samaki kutoka
 Sokoine University of Agriculture
 +255752799673 / 0655859810
Kwa mahitaji ya ushauri, utengenezaji na utunzaji wa mabwawa ya samaki wasiliana nasi


 Kambale (Claries gariepinus), ni aina ya samaki ambao wanafugwa kwenye maji baridi na wana uwezo wa kustahimili mazingira magumu ukilinganisha  na samaki wengine.Samaki hawa wapo spicies au wanatajwa kwa majina mbalimbali kulingana na eneo na jamii husika majina hayo ni  kama vile, kambale channel, koleo, samaki kidevu, samaki wa kwenye matope. n.k. 
          Samaki hawa (kambale) wanakua kwa kiasi kikubwa sana hadi kufikia uzito wa kilo 3 na kuendelea. Kambale hawana magamba na wana uwezo wa kustahimili upungufu mkubwa wa oxygen kwenye maji ya bwawa kwa sababu kibiolojia wana mifumo miwili ya upumuaji katika mwili wao.

                                   ASILI YA KAMBALE

Asili ya samaki hawa ni Amerika ya Kaskazini. Samaki hawa hukua kwa haraka sana, na kuwa na uzito mkubwa. Aina hii ya samaki hupendwa na watu wengi kwa kuwa nyama yake ina ladha nzuri na ni laini sana na pia ina vitamini A. Samaki hawa huzaliana vizuri zaidi wanapokuwa mtoni au sehemu ambayo wanapata tope. Mfugaji anapokusudia kufuga aina hii ya samaki kibiashara, ni vyema kama ataweza kusakafia bwawa au kutumia nailoni ngumu (dam liner, HDPE) ili kuepuka uharibifu unaoweza kusababishwa na samaki hawa. Kambale wakufugwa kwenye mabwawa hawazaliani kabisa kwani mazingira ya ufugaji wa kwenye mabwawa sio mazuri kwao katika kuzaliana.Hawa wanazalishwa kitaalamu kwa kutumia Hormone na ukuaji wake ni mzuri zaidi kuliko wale wanaozaliana w

UMBILE LAKE

Samaki aina ya kambale wana umbo refu, pia ni wapana kuanzia shingoni, ingawa kichwa ni kidogo, na upande wa mkia ni mwembamba. Samaki hawa wana rangi ya kijivu na wengine nyeusi

AINA YA CHAKULA NA ULISHAJI WA KAMBALE
 
Kambale ni aina ya samaki wanaokula nyama (carnivorous) kwa hiyo chakula chake kinahitaji kiwe na viini lishe vya protini kwa kias kikubwa kwa ajili ya ukuaji kulinganisha na aina nyingine za viini lishe vingine kama kabohaidreti, mafuta na vitamin.Unaweza kulisha kambale kwa kutumia unga wa samaki, maharagwe yaliyosagwa, mahindi, mchele pumba, ngano na bidhaa nyingine. Unaweza kujenga mfumo ambao utawawezesha samaki hawa kupata aina mbalimbali za wadudu, pamoja na majani, ili kusaidia wapate mlo kamili.
Kambale kama aina nyingine za samaki,wanalishwa kwa kuzingatia utaratibu maalumu kama ulishaji wa kuzingatia uzito wake na pia ulishaji wa kuangalia uchangamkiaji na uharaka katika kula (response). Hii inasaidia kuepusha upotevu wa chakula na uchafuzi wa bwawa pindi mabaki mengi ya chakula yanapozama kwenye maji na kuoza ambapo inachangia uimara na usafi wa maji kupungua. 

                UKUAJI NA UVUNAJI WA KAMBALE

Aina hii ya samaki, wakitunzwa vizuri, kwa kuwapatia mazingira mazuri, chakula chenye ubora, maji safi na  yakutosha wanaweza kukua kwa haraka na kuwa na uzito mzuri unaoweza kumpatia mfugaji faida nzuri.Kambale wanaweza kufugwa kwa wingi katika eneo dogo ukilinganisha na samaki wengine kama perege. Unaweza kuanza kuvuna kambale baada ya miezi sita tangu walipopandikizwa kwenye bwawa.

                          SOKO LA KAMBALE

 Jambo muhimu la kufikiria kabla ya kuanza ufugaji wa samaki kibiashara Fikiria ni wapi utapata wateja kulingana na zao unalozalisha (samaki) soko la samaki ni muhimu sana kutiliwa maanani kabla ya kuanza kuzalisha.
Wafugaji walio wengi, wamekuwa wakianzisha miradi ya ufugaji wa samaki kwa kufuata mkumbo bila kutambua kwanza soko watakalozalishia samaki hao. Jambo hili huwafanya wafugaji kuwa na kipato kidogo tofauti na nguvu waliyotumia kuzalisha.
Inapofikia wakati wa kuvuna samaki, kiasi kikubwa huuzwa papo hapo bila kufika kwenye soko halisi, jambo linalosababisha kipato kuwa duni. Ni vyema mfugaji akawa na soko maalumu ambalo atazalishia. Unaweza kuzalisha kwa ajili ya shule, hospitali, vyuo, au taasisi yoyote. Halikadhalika jamii inayokuzunguka na taasisi nyinginezo.
Katika kuhakikisha mfugaji wa samaki anapata faida kubwa ni lazima kuzingatia size ya samaki inayohitajika katika soko husika ili kuepuka kukuza samaki kupita size ya soko ambapo itakua ni hasara kwa mfugaji.Kiasi cha samaki wanaotakiwa kuvuliwa kwa ajili ya soko ni lazima kizingatiwe kwa kukidhi mahitaji ya wateja waliopo. Pia ni lazima kipindi au msimu wa kuvuna samaki kiangaliwe kwa makini mfano kuzingatia kipindi ambacho aina ya samaki unaozalisha wanakua sio wengi sana sokoni na hii inapelekea kutoathiri biashara yako.

            HAYA YAZINGATIWE  KWA UFANISI WA SOKO LA SAMAKI
  • Hakikisha samaki wako katika hali ya usafi na vyombo salama unapovua tayari kwa kupeleka sokoni. Hii itapelekea kuzuia contamination na vijidudu vinavyosababisha magonjwa kama vile bacteria, fungus, na virus ambavyo pia vinasababisha samaki kuoza.
  • Samaki ni bidhaa inayoharibika kwa haraka, hivyo hakikisha unawapeleka sokoni mara tu baada ya kuwavua.
  • Hakikisha gharama za usafiri, utunzaji na uhifadhi, zinalipwa kutokana na bei ya soko.
  •  Kumbuka gharama za uhifadhi wa bidhaa inayoharibika haraka kama samaki ni kubwa, hivyo vua kwa awamu kulingana na mahitaji.
  •  Unaweza kuongeza thamani ya samaki kwa kufanya mambo ya msingi yanayohitajika kwenye uandaaji wa samaki, kama vile kuparua na kutumbua.
  • Unaweza kuwasafisha, na pia kuwakaanga kulingana na soko husika.
  • Kwa kuzingatia mambo hayo machache, mfugaji anaweza kufanya maamuzi sahihi kabla ya kuwekeza kwenye mradi wa ufugaji wa samaki. Pia ni muhimu kuzingatia mahitaji muhimu ya ufugaji wa samaki, ili kuepuka gharama zisizo za lazima.  
Fuatilia mwendelezo wa masomo kuhusu ufugaji wa samaki kila wiki
Godfrey, Christopher Sway Mtaalamu wa Samaki kutoka
 Sokoine University of Agriculture
 +255752799673 / 0655859810.
Reactions:

0 comments:

YouTube

GREEN HOUSE

GREEN HOUSE
BEST DESIGN

Visitors

LIKE US ON FACEBOOK

AGRICULTURE LAND

Mostly Visited