Tuesday, 16 May 2017
BIASHARA NA MASOKO YA ZAO LA MUHOGO

Zao hili la muhogo kitaalamu husifika sana kwa kuwa na kiasi kingi cha wanga na hiyo wataalamu wanaliweka katika kundi la vyakula vya wanga(carbohydrate), mihogo hupendwa sana kutumika kama kitafunwa, ukiwa mbichi au ukiwa umepikwa kwa makabila mengi hapa Tanzania na duniani kwa ujumla na kufanya uhitaji wake uwe mkubwa na pia liwe zao la biashara. katika maeneo mengi ya pwani na kusini mwa Tanzania mhogo hupendwa sana na watu huutumia kama chakula chao kwa mara nyingi.
katika biashara ya mhugo tukianzia kwa wakulima kwa soko lilivyo sasa hasa kwa mikoa ya pwani kwa hekari moja mkulima akiuzia mihogo yake shambani anapata Tsh 3,000,000/=. na pia inaposafirishwa mpaka sokoni wachuuzi mbalimbali huuza mhogo mmoja kuazia shilingi 500-1000 kulingana na ukubwa.


KILIMO BORA CHA ZAO LA MUHOGO

Zao la muhogo ni  muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k. Umuhimu wa zao hili ni kutupatia cahakula na wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula kikuu ambacho kinachukua asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya pwani.

Muhogo hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye maeneo ya mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Vile vile muhogo hustawi vizuri kwenye maeneo yanayopata mvua ya wastani wa mm 750  - mm1200 kwa mwaka. Muhogo hustawi vizuri kwenye ardhi ya kichanga. Vili vile zao la muhogo ni maarufu sana kwa uvumilivu wa hali ya ukame.

  • TEKNOLOJIA ZILIZOPO
Mbegu bora za muhogo

Mpaka sasa hivi kuna aina mbili za mbegu bora ambazo zimathibitishwa kwa wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa, (batobato na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji.
Naliendele Huzaa tani 19 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.Kiroba
Huzaa tani 25 – 30  kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.

  • Mbinu bora za kilimo cha muhogo

Uandaaji wa shamba

Shamba liandaliwe kabla ya msimu wa kuanza. Uandaaji wa shamba bora hufuata hatua zifuatazo:

Kufyeka shamba Kung’a na kuchoma visiki Kulima na kutengeneza matuta .
Uchaguzi wa mbegu bora za kupanda Mbegu zinatakiwa zisiwe na magojwa yeyote, pia chagua mashina ambayo yamekomaa vizuri.

Upanadaji


Kuna njia tatu za upandaji wa muhogo: Kulaza ardhini (Horizontal) Kusimamisha wima (Vertcal)Kuinamisha ( Inclined/Slunted)

Urefu wa kipande cha shina cha kupanda:
Inashauriwa urefu uwe sm 30; lakini urefu wa kipande cha kupanda unategemea sana idadi ya macho yaliyopo kwenye hicho kipande, inashauriwa kipande kiwe na macho (4 – 6).

Nafasi ya kupanda:

Kwa upandaji wa shamba muhogo tupu, shina hadi shina ni mita 1 na mstari hadi mstari ni mita 1.Kwa shamba la mchanganyiko na mazao mengine, inategemeana na zao linalochanganywa; mstari hadi mstari ni mita 2 – mita 4 na shina hadi shina ni mita 1.

Palizi:

 Palizi ya kwanza ifanyike mapema (mwezi 1) baada ya kupanda ili kuepukana na magugu yanayochipua haraka baada ya mvua kunyesha. Ndani ya miezi minne ya mwanzo mihogo haitakiwi kuwa na magugu ili kuepuka ushindani wa mahitaji muhimu (mwanga, mbolea, maji, n.k) kati ya muhugo na magugu. Palizi hufanyika kwa kutumia jembe la mkono au dawa ya kuuwa magugu.Wakati mwingine udhibiti wa magugu kufanyika kwa kutumia majani kwa kutandazwa juu ya udongo.Palizi hufanyika mara 2 – 3 hadi muhugo kukomaa.

Uvunaji:

Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 – 12 tangu kupandwa. Inashauriwa kuvuna katika katika kipindi cha jua; kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo hupungua.

Usindikaji bora

Usindikaji bora wa muhogo unafanyika kwa sababu kuu mbili:

Kurahisisha/kuharakisha ukaushajiKuondoa sumu (cyanide) ilyoko kwenye baadhi ya aina za mihogoKuongeza ubora wa unga utokanao muhogo wenyewe.

Njia bora za usindikaji

 
HAND OPERATED 

POWER OPERATED GRATER

Kwa kutumia mashine aina ya Grater Hii hutoa chembechembe laini za muhogo, ambazo baadae hukamuliwa kwa kutumia kifaa kingine kiitwacho “presser” ili kuondo sumu iliyoko kwenye muhogo. Mashine hii hutumika hususani kwa muhogo mchungu.Kwa kutumia mashine aina ya chipperMashine hii hutoa vipande vidogo vidogo (chips). Mashine hii hutumika hasa hasa kwa ajili ya mihogo mitamu/baridi.

Matumizi ya Muhogo


Muhogo unaweza kupikwa wenyewe kama chakula au kutengeneza ungaUnga wa muhogo unaweza kutengeneza vitu vyotekama vinavyotengenezwa na unga wa ngano kama vile biskuti, chapatti, maandazi, chichili, keki n.k.Pia muhogo huweza kutumika viwandani kutengeneza bidhaa nyingine kama vile wanga.


 MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU

Magonjwa

Kuna magonjwa mawili ambayo ni muhimu sana na yanapunguza uzalishaji wa zao la muhogo.

a) Ugonjwa wa Matekenya au Ugonjwa wa michirizi ya kahawia katika muhogo

Ugonjwa huu ni maarufu kwenye sehemu zenye miinuko iliyo na urefu  chini ya mita 300 na unapatikana kidogo sana kwenye miinuko ya mita 500 na kuendelea ambako uenezaji wake wa kawaida hautokei kabisa.

Visababishi:
Matokeo ya uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba ugonjwa huu ulienezwa na mdudu mweupe au inzi mweupe (whitefly) mwenye mabawa madogo.

Dalili za Ugonjwa
Sehemui zote za muhogo zinaweza kuonyesha dalili za uambukizo wa ugonjwa huu lakini ni vipengele gani vya ugonjwa na ni kwa kiwango gani hutegemea hali ya mzingira, hatua ya kukua kwa mmea kwa kulinganisha.

Kwenye majani

Dalili ya kwanza: Chlorosis rangi ya njani hutokea kwanza pembezoni mwa vena ndogo baadae huathtiri vena ndogo zaidi na inaweza kuwa doa (chlorosis) la rangi ya njano.Dalili ya pili: Rangi ya njano ambayo haihusishwi vizuri na vena isipokuwa katika mbaka ya mviringo kati ya vena kuu kwenye hatua za mwisho za ugonjwa sehemu kubwa ya lamin inaweza isiathirike, majni yenye ugonjwa hubaki yameshikilia kwenye mmea kwa muda wa wiki kadhaa.

Kwenye shina

Huonekana kwenye tisu ya shina changa la kijani, jeraha la zambarau au kahawia linweza kuoneakan nje na kuingia ndani hadi kwenye gamba baaada ya kubandua gome la nje. Pia jeraha la nekrotiki kwenye kovu la shina hutokea baada ya majni kudondoka kutokana na umri wa mmea. Tawi/shina hufa kuanzia kwenye nch kuelekea chini na kusababisha kufa kwa mmea wote.

Kwenye mizizi

Kwa kawaida hutokea baada ya dalili za majani na wakati wa kipindi kati ya uambukizo na kufa, amabpo kifo cha mizizi hutokea kuanzia miezi 5 toka kupandwa. Dalili za mizizi zinabadilika nje ya mizizi na zinaweza kuwa kamakizuizimwanga au shimo au kufa kwenye gome.

Tishu inayo zunguka mshins ina doa la rangi ya kahawia au nyeusi. Wakati mwingine mizizi huonekana kuwa yenye afya kwa nje bila kuwa na matatizo yaliyowazi au bila kupungua ukubwa, lakini ikikatwa huonekana kufainakufa au rangi ya njano.
Uambukizaji na ueneaji

Ugonjwa wa CBSD unaambukizwa kwa njia ya vipandikizi vinavyotokea kwenye mimea iliyoathiriwa vinavyosababisha mmea kuonesha kwenye majani dalili za ugonjwa.

Kwa kuwa muhogo kwa kawaida huzalishwa kwa njia ya vipandikizi ugonjwa huu huingizwa kwenye sehemu mpya zilizopandwa kwa kutumia vipandikizi vilivyoambukizwa.
Kwa aina zinazovumilia sana kwenye hali za mabondeni, dalili mbaya sanahutokea wakati ugonjwa ukigundulika  katika hatua za mwanzo.

Uchunguzi umeonesha kwamba Bemisia afer ni mdudu/kisababishi ambacho ndicho kinachohusiana na maendeleo ya hivi karibuni kuhusu uhamishaji wa visababishi kama “ipomovirus”. Mara nyingine inaonesha nzi weupe (White flies) na kutokana na hali hiyo bado uchunguzi unaendelea zaidi.

Udhibiti/Kuzuia

  Njia ya msingi ya kuzuia/kudhibiti ugonjwa wa CBSD ni kuchagua mbegu kutoka kwenye mimea isiyo na dalili ya ugonjwa.  Ubora wa mashina unahitaji kutunzwa kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza ile iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa kuchipua.ü  Hakikisha kuwa unapanda mbegu bora za mhogo ambazo zinastahimili uambukizo wa magonjwa.ü  Hakikisha kuwa wakati wa uvunaji uonapo hali ya kuoza kwa mizizi ya mhogo ichome moto ili kutokomeza ugonjwa huo.ü  Kuelewa dalili za ugonjwa wa CBSD kwa ajili ya kuchukua tahadhari ya kutokomeza ugonjwa huu.ü  Hakikisha kuwa unaendelea kutunza mbegu bora zinazoonekana kuvumilia magonjwa sana.ü  Hakikisha kuwa shamba la mhogo linakuwa safi kwa ajili ya kupunguza visababishi vya ugonjwa wa CBSD


b) Ugonjwa wa batobato au ukoma wa majani(cassava mosaic disease)

MAJANI YALIOATHIRIKA

MIHOGO ILIYOATHIRIKA NA CMD

Ni ugonjwa ambao ulienezwa kwamara ya kwanza hapa Tanzani mwaka 1894, na baadae uliripotiwa katika nchi nyingine nyingi za Afrika Mashriki, Afrika Magharibi na Afrika ya Kati na sasa unafahamika kuwa upo maeneo yote yanayolimwa muhogo Afrika.

Katika viwango vya kuwepo kwa ugonjwa wa CMD na katika uwingi wa hasara zinazopatikana kutokana na CMD ni kati ya 15% – 20%. Hii ni sawa na tani milioni 15 – 18 zikilinganishwa na makadirio ya shirika la kilimo na chakula  duniani ya tani milioni 85 ya mwaka 1997.

Visababishi
Tangu ugonjwa wa CMD ulipoenezwa kwa mara ya kwanza, visababishi vilichukuliwa  kuwa ni virusi kwa sababu ya kukosekana kisababishi kingine. Kwa hiyo kutokana na kuwa mtazamo huu unalingana na matokeo ya uchunguzi wa awali inaonesha kwamba ugonjwa huu huenezwa na nzi mweupe (white fly).

Pia uchunguzi wa mara kwa mara umesababisha utambuzi wa virusi vya aina mbalimbali na tofauti kama ifuatavyo:

Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya Africa cassava mosaic virusUgonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya Afrika mashariki (East Africa cassava mosaic virus)Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya India (Indian cassava mosaic virus)Dalili za ugonjwa wa batobato (Cassava Mosaic Disease-CMD)
                
Dalili hutokea kwenye jani lenye uwaraza wa michirizi ambazo huathiri       
Sehemu zisizokunjamana za kutolea hewa na hufahamika katika hatua za   
Awali za ukuaji wa jani.

Sehemu za kloritiki hushindwa kutanuka hadi mwisho, hivyo mvutano unaji-
tokeza kutokana na ukuaji usiolingana na jani au majani madogo yaliyoharibika.
Majani yaliyoathirika sana hupungua ukubwa wa umbo, na hujikunja na kujitenga kwa
Sehemu zenye rangi ya njano na zenye rangi ya kawaida ya kijani.

Mmea hudumaa na majani machanga hupatwa na uvimbe.
Kloritiki ya jani inaweza kuwa ya rangi ya manjano nyepesi au rangi inayokaribia nyeupe
yenye kijani kidogo au kupauka kuliko ilivyo kawaida.


 Uambukizaji na uenezaji

Ukoma wa mhogo huambukizwa kwenye vipandikizi vya shina ambavyo kwa kawaidahutumika kuzalishia mmea.Pia huenezwa na inzi mweupe (white fly) aitwae Bemisia tabaci G. Aina mbili za inzi auMbu hao Bemisia (Preisner Hhosny na Aleorodius disperses R) pia huambukiza mihogokatika nchi za Afrika na IndiaUsambazaji wa vipandikizi unaweza kusababisha kuenea kwa ugonjwa wa CMD katikaMaeneo mapya.
              
 UDHIBITI NA KUZUIA

Hatua ya msingi ya uzuia ugonjwa wa CMD ni kwa kuchagua vipandikizi kutoka kwa Mmea ambao hauna uambukizo wowote.Ubora wa mashina unahitajika kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza kwa kung’oa ileMihogo iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa kuchipua.Hakikisha kuwa wakati wa kuvuna mihogo kwa ile iliyoathirika na ugonjwa wa CMDinaangamizwa kwa kuchomwa moto.Hakikisha una elimu ya kutosha juu ya dalili za ugonjwa wa CMD>

WADUDU NA WANYAMA WAHARIBIFU


Cassava Mealy Bug (CMB)

CASSAVA MEALY BUGS
LEAVES AFFECTED BY MEALY BUGS
Wadudu hawa hushambulia kwenye ncha za mashina/matawi kwenye majani machanga. Athari zake ni kwamba majani ynadumaa na kujikusanya pamoja, hivyo basi kupunguza ukuaji wa mmea kwa ujumla. Vile vile urefu kati ya pingili na pingili huwa fupi sana.

Cassava Green Mites (CGM)Wadudu hawa hushambulia majani mapya sehemu za chini. Madhara yake sio makubwa.

White ScalesHawa ni weupe na hujishika kwenye shina na kufyonza maji kutoka kwenye mti wa muhogo. Vili vile wadudu hawa madhara yake sio muhimu.

Mchwa

Hawa hutafuna/hula mashina ya muhogo hasa wakati wa jua kali/kiangazi.
Wanyama waharibifu
Hawa hushambulia muhogo ukiwa shambani kwa kuula, kama vile nguruwe, panya, wezi, n.k

Udhibiti/Kuzuia

Kwa upande wa wadudu wanweza kudhibitiwa kwa njia zifuatazo:
i  Kutumia dawa za kuulia wadudu
ii  Kutumia wadudu marafiki wa wakulima

iii Kwa upande wa wanyama ni kuweka walinzi.Mkulima wa zao la mhogo 
Mr Anthony Mbuja , eneo la Bungu Wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani 
(0715934398).
pia Bw. Anthony analima mazao mengine kama papai, Nanasi, Nyanya, Mhindi pia ni mfugaji wa samaki 
na Anahudumia na Kampuni ya Green Agriculture Company ambayo inatoa huduma za ushauri na uuzaji wa bidhaa na pembejeo za kilimo kama mbegu,mbolea,madawa, drip irrigation, Green house,kupima udongo, Ujenzi wa miundombinu ya kuvuna maji ya mvua n.k                                Soma zaidi kuhusu fursa ya zao hili
Octavian Justine Lasway 
Irrigation and Water resources Engineer
0763347985/0673000103

Reactions:

0 comments:

YouTube

GREEN HOUSE

GREEN HOUSE
BEST DESIGN

Visitors

LIKE US ON FACEBOOK

AGRICULTURE LAND

Mostly Visited