Sunday, 7 May 2017


 FURSA KUBWA KWENYE KILIMO CHA STRAWBERRY, MASOKO NA UTAALAMU

  Na

Agronomist Lydia Gerald

0659431884/0620530840

Utangulizi

strawberry (fukasidi) hustawi katika maeneo yenye joto la wastani, na hukua kwa haraka zaidi na uzalishaji kuongezeka linapolimwa kisasa zaidi, Hasa katika  Green house. Zao hili hukua vizuri katika mwinuko wa mita 1500 na zaidi kutoka usawa wa bahari. Zao hili hata Tanzania hustawi zaidi katika mikoa mingi kama Morogoro,mbeya,iringa, Arusha, Kilimanjaro, na Pia hufanya vizuri katika mikoa ya Pwani endapo utalima kisasa zaidi na kufuata maelekezo ya kitaalamu(Under controlled condition)

Udongo

strawberry inaweza kustawi vizuri kwenye udongo tifutifu wenye rutuba. Zao hili haliwezi kustahimili ukuaji kwenye udongo wenye chachu nyingi, hasa chokaa kwani mizizi yake huoza kwa urahisi, Pia udongo unaotuamisha maji kama mfinyanzi sio mzuri sana kwa ustawishaji wa strawberry, Pima Udongo kabla ya kuanza kilimo sio kwa strawberry peke yake hata kwa mazao mengine 

Kupanda

Ili kuwa na mazao bora ambayo yatakuwezesha kupata soko la uhakika,  inashauriwa kuzalisha kwenye nyumba maalumu ya kuzalishia mazao (green house). 
1. Katika upandaji wa strawberry kwenye green house Utahitajika kuwa na Mabomba yenye matundu(Plastic Pipe)
  Matundu katika bomba hilo yawe na umbali wa inchi 1.
2.  Ni vyema matundu hayo yakawa zigzag, ili kuruhusu mimea utakayoipanda kukua vizuri bila kusongamana
        3. Tandika karatasi la nylon sakafuni ili kuwezesha maji utakayotumia kunyeshea kurudi kwenye bwawa au
sehemu ya kuhifadhia.
        4.Ning’iniza mabomba hayo kwa kutumia waya.
       5. Jaza kokote, yenye mapande makubwa kiasi.
       6 .Panda miche kwenye kila tundu kwa uangalifu ili mizizi isikatwe na kokoto zinazoshikilia mmea

                                        Kupanda Kwenye Shamba la Kawaida
 umwagiliaji

Mimea ya strawberry inahitaji maji kwa kiasi kikubwa sana. Hii inamaanisha kuwa unahitaji kuwa na mfumo mzuri
wa umwagiliaji kabla ya kuanza kilimo cha zao hili. Unapaswa kumwagilia mara nne kwa siku, kila baada ya saa nne unapaswa kumwagilia kwa robo saa. Hii itawezesha mimea yote kupata maji ya kutosha. Endapo stroberi haitapata maji ya kutosha, uzalishaji wake pia utakuwa ni hafifu sana, kwani maua hayatachanua ipasavyo na hata matunda kukomaa inakuwa ni shida.

Kuvuna

Zao la strawberry  huzaliana na kukomaa kwa haraka sana. Unaweza kuanza kuvuna stroberi baada ya mwezi mmoja tangu kupandwa. Kila wiki stroberi inakuwa na matunda mapya, na kila tunda likishatokeza huiva kwa haraka, hivyo uvunaji wake ni wa mfululizo ikshafikia hatua hiyo tegemea kuwa na wiki 2-3 za kuvuna mfululizo.
Kwa kuwa matunda ya stroberi ni laini, epuka kushika tunda wakati wa uvunaji ili lisiharibike. Shika kikonyo
cha tunda ili kuvuna kwa usalama. Usiache matunda yaliyoiva shambani kwa muda mrefu kwani yanaweza
kusababisha mimea kuoza. Pia yatapoteza ladha na virutubisho halisi vinavyotakiwai

Wadudu na magonjwa

Endapo strawberry inazalishwa kwenye nyumba maalumu ya mimea, hakuna magonjwa wala wadudu wanaoishambulia. Ikiwa mkulima anazalisha stroberi kwenye eneo la wazi, stroberi inaweza kushambuliwa na magonjwa ya ukungu, pamoja na magonjwa yanayosababishwa na virusi. Kama vile;

(  Wadudu

b.  Heliothis
c.  Looper
e.  Cutworm
f.  Aphids

(  Magonjwa 

   Lethal yellows

Mmea ulioathirika unaonyesha dalili zifuatazo;
   Majani yaliyokomaa yanakuwa na rangi ya dhambarau na yanajinyonganyonga kwa upande wa juu na kusababisha kuangua chini.
Majani chipukizi yanakuwa na rangi ya njano katika kingo za jani na kupelekea kudumaa kwa kikonyo cha jani. Huu ugonjwa unapunguza nafasi ya jani kushindwa kujitengenezea chakula chake na hivyo mmea kudumaa na kupelekea kufa kwa mmea.

Mnyauko fusari (fusarium wilt)

Huu ugonjwa huunezwa na mbegu zenye huu ugonjwa na husambazwa na vimelea vya fangasi ambavyo vipo kwenye udongo.
Ugonjwa huu hujitokeza Zaidi kwenye kipindi cha kiangazi na hushambulia sehemu za mirija yam mea ya kupitishia chakula hivyo mmea hukosa chakula na maji na hatimaye unyauka na kufa. Na shina la mmea ukipasua ndani unakuta lina rangi ya kahawia.
Kudhibiti
1.  Tumia mbegu safi na bora.
2.  Tumia dawa ya kuua wadudu na magonjwa ili kupata mazao mengi na yenye ubora.
3.  Choma masalia ya mazao ili kudhibiti uenezaji wa ugonjwa
4.  Chagua mbegu ambayo ina uwezo wa kuhimili magonjwa.

Matumizi ya strawberry

Matunda ya strawberry yana matumizi mbalimbali kulingana na uhitaji wa mtumiaji, jamii na maeneo.
Miongoni mwa matumizi hayo ni pamoja na  

  1.   Kuliwa kama tunda
  2.   Kutia ladha katika aina mbalimbali za vyakula.
  3.   Kuweka rangi, harufu na nakshi katika vipodozi.
  4.   Kutengeneza marashi n.k.
strawberry inapooteshwa kwenye greenhouse hutoa mavuno mengi na yenye ubora. Wasiliana na wataalamu wa green agriculture kwa ajili ya ujenzi wa green house kwa ajili ya uzalishaji bora wa strawberry.
Mkulima wa Straberry 
Hassan Yakubu maarufu kama King Of Straberry Akiwa shambani Kwake Morogoro
 HAYATE ORGANIC 
 FARMS 
  &
       GREEN        
    AGRICULTURE 
       COMPANY 
Kwa mahitaji ya ushauri, mbegu na biashara ya straberry wasiliana nasi kwa number zifuatazo 
Hassan Yakubu(0716508848) na Agronomist Lydia Gerald 0659431884/0620530840


Reactions:

0 comments:

YouTube

GREEN HOUSE

GREEN HOUSE
BEST DESIGN

Visitors

LIKE US ON FACEBOOK

AGRICULTURE LAND

Mostly Visited