Wataalamu
ABDUL MKONO (MWL ABUU)
BSc AEA, SUA
a2mkno@gmail.com
a2mkno@gmail.com
0767359818 /0652359818
Eng OCTAVIAN J LASWAY
IRRIGATION AND WATER
IRRIGATION AND WATER
0763347985/0673000103
Naitwa KULTHUM kutoka DODOMA
kutokana na nakala zako nzuri za kilimo kama hiyo ilopita ya mbolea ningependa
kujua jinsi ya kuandaa udongo kwa ajili ya kitalu cha kisasa (Seedling Trays).
Kwa ajili ya kusia mbegu zangu za nyanya.
MAJIBU: Kuna
baadhi ya mazao ambayo kama mkulima huwezi kuyapanda moja kwa moja shambani
lazima kwanza uweze kuyaandaa katika kitalu ili yahifadhiwe kwa muda maalumu
(Mara nyingi sio chini ya wiki tatu kwa mazao ya matunda na mboga mboga). Kisha
kuhamishwa shambani yakiwa na afya. Sasa katika maandalizi ya kuandaa mmea
kitaluni zipo njia kuu mbili za kuandaa mmea katika kitalu. Njia hizo ni:-
1. Kitalu
cha kisasa
2. Kitalu asili
1. KITALU CHA KISASA: Kitalu
hichi huandaliwa katika plastiki maalumu ambazo zina matundu (Seedling Trays). Plastiki
hizi huwekewa udongo maaulumu katika matundu hayo kisha mbegu huwekwa katika
udongo huo kwa ajili ya kukuzwa. Huu udongo huuzwa lakini pia kuna njia maalumu
za kuuandaa udongo huo. Na hapa ndo swali lako lilipo.
Kuandaa
udongo huu unapaswa kuandaa vifaa vifuatavyo:-
1. Udongo
2. Mchanga
3. Samadi
4. Majani
yaliyooza (Humus)
Udongo
unapaswa kuwa mara nne (4) ya mchanga, samadi, na majani yaliyooza (Humus). Kwa
mfano: kwa mkulima mwenye mbegu 2500 za nyanya ataanda udongo kilo 30, mchanga
kilo 7.5, samadi kilo 7.5 na ,majani yaliyooza kilo 7.5.
Mara
baada ya kuwa na vifaa hapo juu utachanganya udongo, mchanga, samadi na majani
yaliyooza kwa pamoja kisha chukua maji uchanganye mchanganyiko huo. Kiasi cha
maji kiwe kidogo kiasi cha kupata tope dogo tu. Kisha baada ya hapo udongo huo
utawekwa katika matundu hayo kisha unachukua kifaa kikali na chembamba kama
spoku kwa ajili ya kutoboa katika udongo huo ili kupata nafasi ya mbegu ambayo
itawekwa na kufukiwa na kiasi cha udongo kilichotolewa. Kwa kawaida udongo
unaotolewa ni kidogo tu mfano wa mbegu husika.
Baada
ya mbegu kuwekwa katika tray hizo itafunikwa na nailoni nyeusi kwa muda wa siku
tatu ukiwa unachunguza kama mbegu imeshaota. Ukiona mbegu zishaota ondoa
nailoni nyeusi kisha chukua trei hizo uziweke mahali ambapo pana kivuli kama
chini ya mti au tengeneza kichanja. Hapa utaendelea kumwagilia maji asubuh na jioni
mpaka siku ya kuhamisha. Wiki moja kabla ya uhamisha shambani punguza
umwagiliaji na siku ya kuhamisha usimwagilie kabisa ili uweze kuhamisha mmea na
udongo wake.
KUMBUKA:
Umwagiliaji ufanyike pole pole sana kwani ukifanyika haraka waweza kuondoa
udongo na siku ya kuhamisha mmea ukahamishwa bila ya udongo wake. Lakini pia
ikitokea mkulima amekosea kuchanganya udongo kwa uwiano sahihi nilioelekeza
inaweza kupelekea mmea kushindwa kuhamishwa na udongo wake. Lakini pia kama
mkulima akishindwa kuandaa udongo huu atapaswa kununua udongo maalumu kwa ajili
ya kusia mbegu. Udongo huo pia ni mzuri na utamsaidia mkulima kuhamisha mmea
wake shambani ukiwa na udongo.
Picha
ya kwanza kushoto kitalu cha kisasa kikiwa na udongo uliotengenezwa kwa uwiano
nilioelekeza pale juu. Na kulia ni picha ya kitalu cha kisasa.
2. KITALU ASILIA: Kitalu
hiki hutumika na asilimia kubwa ya watanzania kutokana na maandalizi yake ni mepesi.
Huandaliwa kwa kunyanyua tuta kimo cha sentimeta ishirini. Kisha huwa na upana
wa mita mbili na urefu kutokana na idadi ya miche husika. Kisha tuta hilo
huandaliwa vifereji ambavyo vitaachana sentimita 20 kuelekea upana ulivyo. Na
vifereji hivyoh huwekwa mbolea na kulowanishwa. Kisha mbegu humwagwa katika
vifereji hivyo na kufukiwa vyema. Baada ya hapo kitalu choote hufunikwa na
matandazo ili kuhifadhi unyevu. Baada ya siku tatu miche ikiwa ishaanza kutoka
utaondoa matandazo kisha utaweka kichanja. Baada ya siku 21 au zaidi mmea
utakuwa na afya kwa ajili ya kuhamishwa shambani. Hapa utahitajika kupunguza
umwagiliaji wiki moja kabla ili kuuandaa mmea kwa ajili ya kuhamishwa shambani.
Changamoto kubwa ya kitalu hiki cha asili baadhi yam mea itashindwa kuhamishwa
shambani ikiwa na udongo hivyo kupelekea kufa ikiwa shambani. Angalia picha ya
kitalu cha asili:-
Wataalamu
ABDUL MKONO (MWL ABUU)
BSc AEA, SUA
a2mkno@gmail.com
a2mkno@gmail.com
0767359818
0652359818
Eng OCTAVIAN J LASWAY
0763347985/0673000103
1 comments:
Wataalamu ni njia gani rahisi ambayo naweza kutumia ili kupata makala au post zenu. Utaalamu wenu umeenda shule haswaaa.
Post a comment