Friday, 31 March 2017

 MASWALI NA MAJIBU KUTOKA KWA WAKULIMA WETU


Wataalamu 
ABDUL MKONO (MWL ABUU)  
BSc AEA, SUA                      
 a2mkno@gmail.com 
 0767359818 /0652359818
Eng  OCTAVIAN J LASWAY
IRRIGATION AND WATER
0763347985/0673000103
Naitwa LEAH PETER nipo Dar es salaam
a) Ni upi umuhimu wa buster kwa mazao ya matunda na mifano yake?
b) Je ni kweli kuwa mbegu za tikiti lazima kuloweka?
c) Je kuna kipimo sahihi cha maji kinachopaswa kumwagiwa mmea wa tikiti maji katika ukuaji wake?

Kiasi cha maji yanayohitajika kwa mmea wowote ule hutegemeana na mambo mengi. Ila mambo muhimu ni aina ya udongo na hali ya hewa ya eneo husika. Mfano maeneo ambayo kuna udongo wa kichanga na jua kali mmea hupoteza maji mengi sana hewani hivyo hapa mkulima atahitajika kumwagia maji mengi sana asubuhi na jioni ikiwezekana kila siku. Tofauti na mtu mwenye udongo wa kitifutifu na maeneo yasiyo na jua kali. Na ndio maana kumsaidia mkulima tunaanza na kupima udongo wake kisha ndo tunakupa ratiba sahihi ya umwagiliaji. Tofauti na hapo utakuwa unabahatisha na maji yakizidi mmea wako utaathirika na ugonjwa wa kata kiuno angalia picha chini.
Picha ugonjwa wa kata kiuno (Damping off)
Na ikitokea maji yapo kidogo uzalishaji utapungua. Lakini napenda kueleza uhitaji wa maji katika mmea kwa kipindi tofauti tofauti cha ukuaji wake.
MAENEO AMBAYO MAJI HUHITAJIKA KWA WINGI KATIKA ZAO LA TIKITI
Ø  Kabla mmea haujaoteshwa shamba linapaswa kumwagiliwa maji siku mbili mpaka tatu.
Ø  Lakini pia mmea ukishaoteshwa huhitaji maji,
Ø  Unapotoa majani unahitaji maji,
Ø  Unapotoa mauwa unahitaji maji,
Ø  Unapotoa tunda unahitaji maji,
Ø  Tunda linapoanza kukomaa mmea hauhitaji maji ili uweze kutengeneza ladha nzuri. Kipindi cha kukomaa tunda ukizidisha maji  tunda lako linakosa ladha.
KUMBUKA
Kipindi ambacho mmea hupoteza maji yake kupitia stomata (evaporation) haswa kipindi cha jua kali na mvua ikawa ndogo mkulima awe makini sana na ratiba yake ya umwagiliaji maana hapo mmea huhitaji maji lakini katika maeneo niliyoelezea.


 Naitwa YOABU SAMAJE ninalima nyanya na hoho nina swali moja kuhusiana na upunguzaji wa matunda kwa kila mmea je unahitajika upunguze matunda yakifika hatua ipi?

Mimea tofauti tofauti huweza kupunguzwa majani kwa lengo la kusaidia mmea kuweza kuhudumia matunda ili yawe na afya njema. Tukianza na zao la tikiti mmea ukiwa ushatoa matunda makubwa matatu mkulima hushauriwa kufanya yafuatayo:-
a) Kukata liwe tawi lenye matunda matatu mbele ya matunda hayo.
b) Kukata tawi linguine lolote lile ambalo litakuwa limeongeza zaidi ya matunda matatu ambayo yashakuwa na afya inayoonekana.
KUMBUKA: Mmea wa tikiti hupaswa kuwa na matunda matatu ambao utaweza kuyahudumia vyema. Matunda yatakayoongezeka baada ya yale ya tatu yatapaswa kuondolewa kwa kuyakata na kisu kikali au kukata mmea woote unaoongezeka urefu wakati nyuma ya mmea huo kuna matunda matatu utapaswa kukatwa. Mkulima akate kwa kisu kikali na aepushe kuumiza mmea na pia awe na mikono misafi ikiwezekana anawe kabla hajaanza kazi hiyo.
Tukija kwenye mmea wa nyanya kupunguza majani hufanywa kwa kupunguza baadhi ya vishina vidogo vidogo vitakavyokuwa vinaota kwenye shina kuu. Ili kuruhusu shina kuu kuendelea kutoa mauwa ambayo yatakuja kuwa matunda baadae. Kuruhusu mmea kuendelea kuzaa vishina vidogo vidogo vinavyotokeza katika shina kuu hupelekea mmea kushindwa kuzaa nyanya zenye afya na kubwa hii pia hufanyika katika hoho. Angalia upunguzaji wa majani katika nyanya.

Karibu kwa huduma za umwagiliaji kama drip irrigation na sprinkler, pia huduma ya kupima udongo, green house na net house, pia kwa wanaohitaji materials zote za kilimo pamoja na mbegu

ABDUL MKONO (MWL ABUU)  
BSc AEA, SUA                      
 a2mkno@gmail.com 
 0767359818 /0652359818

Eng  OCTAVIAN J LASWAY
IRRIGATION AND WATER
0763347985/0673000103

Reactions:

0 comments:

YouTube

GREEN HOUSE

GREEN HOUSE
BEST DESIGN

Visitors

LIKE US ON FACEBOOK

AGRICULTURE LAND

Mostly Visited