Monday, 6 March 2017
Wataalamu 
ABDUL MKONO (MWL ABUU)  
BSc AEA, SUA                      
 a2mkno@gmail.com 
 0767359818 
0652359818
Eng  OCTAVIAN J LASWAY
0763347985/0673000103
Mtaalamu kutokana na ufuatiliaji wa Makala zenu toka mwanzo nahitaji kujua muda maalumu wa kulima zao la kitunguu na tikiti maji na gharama zao kwa ujumla kwa ekari moja maana nakumbuka ulisema tatizo mojawapo la wakulima kushindwa kufanikiwa katika kilimo ni kutokujipanga kirasilimali pesa na kutokujua masoko na kipindi chake. Jina langu ni NOAH MUDYAHELA kutoka KILIMANJARO.

MAJIBU:
Kwa zao la kitunguu mnaweza kuanza kuandaa mashamba mwezi wa tano mwishoni hivi ili mwezi wa sita mwanzoni msie mbegu kitaluni, ambapo miche itakaa kitalauni mpaka mwezi wa saba katikati au mwishoni, kisha miche itakwenda shambani wiki ya kwanza ya mwezi wa 8, ambapo utavivuna mwezi wa 10 katikati. Kisha utavihifadhi mpaka mwezi wa 11 mwishoni/December mwanzoni utaanza kupata bei nzuri angalau gunia moja la kilo 100-120 utaanza kupata tsh 100,000-150,000. Mavuno ni gunia kuanzia gunia 70-80 kwa uchache mpaka gunia 120. Hivyo ujiandae kupata kiasi cha Tshs 7,000,000 mpaka 8,000,000 na zaidi au pungufu pia hii yoote hutokana na matunzo na jinsi ya kuhudumia shamba Kama ushauri kutoka kwa wataalaumu na kupima udongo. Na hiyo ni bei ya faida kwani kuhusiana na swali lako la kujua gharama huwa haizidi milioni mbili na nusu (2,500,000) angalia jedwali hapo chini.Kwa zao la tikiti maji, maandalizi ya shamba yanaweza kuanza mwezi wa saba, ili uweze kuzipanda mwezi wa 8 katikati. Hapa utakuja kuvuna mwezi wa 10. Tikiti hizi za mwezi wa 10 zinabei nzuri sana maana wakati huo ni kiangazi mnoo nchi nzima, kwa hiyo wale wapambanaji watakaokabiliana na ukame kwa kumwagilia maji, basi mwezi wa kumi mpaka wa kumi na moja tikiti pia huwa na bei nzuri sana. Lakini pia tikiti za mwezi wa tatu mpaka wa nne (Wakati wa masika) pia soko lake huwa zuri kwani kuzalisha kipindi cha mvua kuna changamoto kubwa na wengi hukwama. Huingia miche 2000 mpaka 3000 na ukisimamia vyema unaweza pata matunda 200-3000 yenye kilo 8-12 na kila tikiti kwa bei shambani tsh 1800-2500. Waweza pata 3,600,000 mpaka 7,500,000. Na kwa ekari moja gharama ni kama ths 1,630,000/- hivyo waweza ona wapata faida nzuri sana ndani ya siku 75. Angalia mchanganuo wa gharama za tikiti hapo chini katika jedwali

KUMBUKA;
Mavuno ya mazao yeyote yale hutegemeana na usimamizi uliokuwa bora katika menejimenti watu, madawa, mbolea na rasilimali pesa kwa ujumla. Kwa kuwa mambo haya hutofautiana baina ya wakulima katika maandalizi ndio utakuta hata mavuno huja tofauti pia. Kuhusiana na gharama hapo juu huweza kuongezeka kidogo au kupungua kutokana na eneo husika, wafanyakazi, au msimu.
Reactions:

0 comments:

YouTube

GREEN HOUSE

GREEN HOUSE
BEST DESIGN

Visitors

LIKE US ON FACEBOOK

AGRICULTURE LAND

Mostly Visited