Saturday, 11 March 2017

Agronomist Lidya Gerald
Phone: 0659431884
Green Agriculture company

Utangulizi
Viwavi jeshi (Helicoverpa ssp) ni hatua ya lava wa kipepeo katika ukuaji wake.
Wanakula majani kwa wingi na kusababisha mmea kushindwa kujitengenezea chakula chake kwa ajili ya ukuaji wake.
Ni adui mkubwa kwa mkulima kwa sababu wanashambulia mimea mengi kama mahindi,pamba, mbaazi, dengu, nyanya, mtama , kunde n.k
Wanatabia ya kukua kwa haraka mno kipindi cha kipupwe.

Mzunnguko wa maisha

Ni imani iliyowekwa kwamba vipepeo huishi kwa mda mfupi sana kuanzia wiki moja hadi takribani mwaka mmoja kulingana na maisha yao hivyo ni muhimu kujua hatua za mdudu huyu ili kutusaidia kutambua ni hatua ipi ambayo hushambulia mazao yetu na kutafuta njia sahihi ya kudhibiti ili asiendelee kuharibu mazao yetu.
Mzunguko una sehemu 4 ambazo ni;
Yai
Kipepeo anauwezo wa kutaga mayai (fertile eggs) kwenye majira ya baridi (kipupwe) siku 6 hadi10 na kwa upande kiangazi (25°C) ndani ya siku 3.
Kiwavi (lava)
Kiwavi wa kipepeo hula majani kwa wingi na hutumia mda wao wingi kutafuta chakula na wachache wao hula wadudu, kiwavi anapitia instar 6 na kukamilisha ukuaji wake ndani ya wiki 2 hadi wiki ya 3 wakati wa kiangazi au ndani ya wiki ya 4 hadi 6 kipindi cha masika. Na kwenye hatua hii viwavi jeshi huwa wanauwezo wakuzalisha  kimekali fulani na kutumika kama ulinzi kwao.
Hii ni hatua hatari sana kwa mkulima kwa sababu ni hatua ambayo viwavi jeshi wanakula majani na kushambulia zaidi sehemu nyingine muhimu za mmea kama podi,mbegu ,maua, machipukizi ya mmea, na matunda. Ni muhimu kujua 90% ya uharibifu unafanywa na hatua hii kuanzia instar ya 3 na kuendelea.
Bundo (pupa)
Kiwavi anapokuwa na kukamilika, kuna homoni kadhaa huanza kuzalishwa wakati huu, kiwavi huacha kula na kuanza kutafuta sehemu na kutulia mara nyingi huwa chini ya majani. Hatimaye kiwavi hubadika kuwa bundo. Bundo kwa kawaida hajongei na isipokuwa huweza kujitikisa au kujinyonga nyonga na kutoa milio kadhaa kuwatishia wadudu.  Hii hutokea ndani ya wiki 2 kwa upande wa kiangazi   na wiki 6 kwa upande wa masika.
Ndumili (imago)
Baadae bundo hukua na kupitia mabadiliko katika mfumo wa metamofosisi na kuwa kipepeo kamili.katika hatua hii kipepeo huitwa ndulimi. Hii hatua hukamika ndani ya siku 10.


Jinsi ya kudhibiti

1.Nyunyuzia dawa ya kuua wadudu mfano cypermethrin, deltamethrin, chlorpyrifos, dicofol, triazophos, thiodicarb, methomyl.
2.Fanya mzunguko wa mazao (crops rotation). Usipande zao sehemu moja kila msimu
3.Unatakiwa kutumia mbegu safi na bora
Panda mbegu zinazohimili ugonjwa
4.Teketeza masalia ya mimea
Agronomist Lidya Gerald
Phone: 0659431884
www.greenagricultureskills.com
Reactions:

2 comments:

Unknown said...

Nice msg short and clear

Unknown said...

UBARIKIWE SANA

YouTube

GREEN HOUSE

GREEN HOUSE
BEST DESIGN

Visitors

LIKE US ON FACEBOOK

AGRICULTURE LAND

Mostly Visited