MASWALI NA MAJIBU
Moja kwa moja katika kuboresha kilimo tunawaletea maswali na majibu kama mlivyo uliza kwenye mitandao ya kijamii na magazeti
Wataalamu
ABDUL MKONO (MWL ABUU)
BSc AEA, SUA
Email : a2mkno@gmail.com
Phone 0767359818
0652359818
ENGINEER OCTAVIAN J LASWAY
BSc. IRRIGATION AND WATER RESOURCES ENGINEERING
SUA
0763347985/0673000103
1. Kwa majina naitwa FRANK MSHANA natokea DODOMA nalima nyanya katika green house. Kuna ugonjwa unanisumbua sana Mtaalam kama unavyoona hapo katika picha. Je dawa yake ni ipi?
JIBU;
Ugonjwa huo
husababishwa na virusi viitwavyo kwa jina la kitaalamu Tomato leaf curl virus.
Virusi husambazwa kutoka mimea iliyoathirika na kwenda kwenye mimea yenye afya
kupitia kufyonza kwa nzi weupe (whiteflies), (thrips) na wadudu mafuta
ambao kitaalamu huitwa (aphids). Hivyo hakuna kinga maalumu
ya virusi huyu ispokuwa kuzuia mashambulizi ya ugonjwa huu kuendelea kuenea
maana huenea haraka sana. Kuzuia kuenea haraka tafuta dawa ya kupambana na inzi
weupe, wadudu mafuta au thrips dawa hizo zipo nyingi hapa ntataja chache mfano DYNAMEC, ACTARA na nyinginezo mojawapo ya
hizo.
Kwa faida ya wasomaji ugonjwa huu ni hatari sana hivyo bora mkajua dalili
ya ugonjwa huu ili kuweza kukinga mara baada ya kuziona.
DALILI
Dalili zinajumuisha mmea kuwa na rangi ya manjano, mabaka, rangi za
kahawia, kudumaa, kukunjika kwa majani, nafasi fupi baina ya vifundo, majani
membamba. Mazao duni, kuchelewa kuiva kwa matunda, rangi isiyo sawasawa ya
matunda ni matokeo ya mashambulizi. Lakini pia dalili za ugonjwa hutegemeana
sana umri wa mmea ulioshambuliwa, hali ya mazingira, aina au jamii ya virusi
vilivyopo lakini pia aina ya nyanya pia.
Lakini pia mkulima ni bora afuate mbinu zifuatazo mapema kabisa ili aweze
kujikinga na ugonjwa huu kwa sababu pindi uingiapo shambani hupunguza
uzalishaji.
MBINU BORA ZA KILIMO
v Fuata
ratiba maalumu za upigaji wa dawa katika vipindi tofauti tofauti vya ukuaji wa
mmea ili kukinga magonjwa hatarishi kwa mmea. Kitu ambacho wakulima wengi
hawana ratiba hizo na wala hawazijui.
v Panda
nyanya zilizokingwa na epuka mbegu za asili hasa za kukamua.
v Tumia
chandarua au neti maalumu katika kuhifadhi miche isigusane na wadudu.
v Epukana
na ardhi iliyolimwa nyanya kwa muda mrefu na zenye mimea iliyoathirika.
v Ng’oa
mimea iliyoathirika na choma moto mabaki ya mazao.
v Fanya
mzunguko wa mazao na mimea yenye kustahimili.
v Epuka
kuvuta sigara wakati wa kuhudumia nyanya.
v Safisha
mikono na zana kwa kutumia dawa za kuua vimelea vya magonjwa na epuka kwenda
kwenye mashamba safi baada ya kutoka kwenye mashamba yaliyoathirika.
KUMBUKA
Mkulima unapaswa kujua
ratiba maalumu ya upigaji dawa na sio kukurupuka mara baada ya kuona ugonjwa
umeingia shambani. Wakulima wengi hukurupuka na kusahau kuwa ugonjwa huu
ukishauingilia mmea hamna namna ya kuuokoa zaidi ya kuuondoa na kuuchoma. Na
hapa mkulima anakuwa anaingia katika hasara maana hata idadi ya matunda
yanayotegemewa kuvunwa hupungua.
2. jina langu naitwa DEOGRATIUS MAKISHE nipo Arusha, swali langu kuhusiana na mada iliyopita ya mbolea ya maji. Je mbolea ya maji inaweza kudumu kwa muda gani na njia gani sahihi ya kuhifadhi mbolea hiyo bila kuharibika?
MAJIBU: Mbolea ya maji huweza kudumu kwa muda wa siku
saba tu na hapo huwa imeshaoza vyema na tayari kwa matumizi. Na ndio maana ili
mkulima aweze kuweka mbolea kwa siku saba mfululizo anapaswa kuwa na madumu
saba ili kila moja likikamilisha siku linatumika na kisha kuandaliwa upya. Ni
vyema ikae siku saba kwani mbolea itakapolowekwa zaidi ya siku saba kuna
uwezekano ikaleta wadudu waharibifu.
Kuhusiana na kipengele
kinachosema kuwa njia sahihi ya kuhifadhi. Kikubwa inapaswa kufunikwa ikiwa
inaandaliwa na inapokamilisha siku saba yapaswa kutumika mara moja. Haitofaa
useme utatazalisha mbolea nyingi sana ili upumzike na kuanza kuitumia labda kwa
mwezi hivi. Jibu ni hapana kila wiki unapaswa kuandaa mbolea hii ambayo itakuwa
ikitumika kila siku.
Usikose kusoma gazeti la mwananchi kila jumamosi ukurasa wa 33 ili ukutane na makala nzuri zenye kusheheni ujuzi na utaalamu wa kilimo
bonyeza hapa kusoma makala nyingine kama drip irrigation system, Umuhimu wa kupima udongo
0 comments:
Post a comment