Sunday, 30 October 2016

MWONGOZO WA KILIMO BORA CHA BEETROT 


MWONGOZO
WA KILIMO BORA CHA BEETROT

Na. ABDUL A. MKONO (MWL ABUU)
Bsch AEA, SUA
UTANGULIZI

Ili kupata chakula chenye madini ya kutosha na ya kufana wataalamu hushauri tule matunda na mboga mboga kwa wingi. Na mojawapo ya vyakula hivi ni tunda au mmea aina ya beetroot kama unavyofahamika zaidi kwa kimombo.

Beetroot ni zao ambalo jina lake kibaiolojia huitwa Beta vulgaris. Na zao hili tunda lake hujiunda katika mizizi kama kitunguu. Beetroot ni muhimu sana kwa kuongeza damu na kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali. Inaweza kuliwa kama ilivyo baada ya kuvunwa au ikatengenezwa juice na ikatumika vizuri kabisa.

Lakini  pia majani yake yanalika kama spinach. Kwa ukuaji bora wa mimea hii inahitaji mvua ya kutosha. Pia hukubali vyema katika udongo wenye rutuba na wa kitifutifu. Udongo wa mfinyanzi ambao ukikauka unapasuka husababisha tunda kuwa na umbo ambalo sio zuri kibiashara.
 

Picha: Mwonekano tofauti tofauti wa aina za beetrot

MAHITAJI YA UDONGO

Zao hili husawi zaidi katika udongo wenye uchachu uchachu (soil ph) kuanzia 5.8-8.0 na kama udongo utakuwa haujapimwa ni bora mkulima akapima ili ajue kwa kuwa kama udongo una asidi nyingi utaathiri sana ukuaji wa zao hili kwa kusababisha upungufu wa virutubisho muhimu.

KUANDAA SHAMBA

Mbegu huoteshwa shambani kabisa wala hamna haja ya kusia mbegu. Hivyo hapa nakushauri ndugu mkulima ulime vizuri kwa kuondoa majani, visiki, na takataka zoote na utifue vizuri kina cha sm 15-20, vunja vunja kasha sawazisha shamba lako. Baada ya hapo nyanyua matuta juu ili kuweka mzunguko mzuri wa hewa na pia njia nzuri ya usafirishaji maji. Udongo uondolewe uchafu woote ikiwemo mimea iliyooza.

KUOTESHA NA NAFASI ZA KUOTESHA
Mara baada ya kuandaa shamba, utachukua mbolea ya samadi ambayo  utaichanganya na udongo wakati wa kunyanyua matuta yako. Kisha baada ya hapo mbegu inapaswa kuoteshwa chini kwenye kina cha sm 1 hadi 2.5 kwenda chini. Kasha mkulima aandae tuta lenye urefu apendao yeye na upana wa mita moja.

Kisha mkulima anaweza kuandaa mstari mmoja akaupanda beetroot zikaachana sm 10, kasha mstari kwa mstari zikaachana sm 20-45. Au
Aweke vijimstari viwili ndani ya tuta moja au vijimstari viatatu ndani ya tuta moja. Nfasi ya mche kwa mche iwe sm 10, mstari kwa mstari kwa mstari sm 20. Na tuta kwa tuta anaweza akaacha hata mita moja. Angalia aina tofauti tofauti za uoteshaji chini.

Mara baada ya kuchimba vijimstari na aoteshe huko mbegu za beetroot kisha afukie na udongo kidogo tena mwepesi ili kurahisisha mbegu kuota. Mara baada ya kuotesha aweke matandazo makavu kisha aanze kumwagilia maji asubuh na jioni baada ya siku 5-12 mbegu zitakuwa zishaanza kuota.


UWEKAJI WA MBOLEA
Uwekaji wa mbolea mara kwa mara ni jambo muhimu mno. Nkiwa na maana kiwango cha naitrojeni kinachowekwa udongoni, fosiforasi na potash kiwekwe mara kwa mara yaani kwa mbolea za dukani ni sawa na kusema uwekaji wa NPK. Ila uwekaji wa mbolea ni vizuri ukatokana na vipimo. Majibu yanasemaje kuhusu kuwepo kwa virutubisho hivyo muhimu vitatu kwenye udongo wako? Kisha sasa anza kuweka mbolea. Mara nyingi huwa namshauri mkulima awe anaweka mbolea asili ya ng’ombe. Ikiwezekana kila baada ya siku saba. Unachukua mbolea ya ng’ombe iliyooza vizuri unarushia katika mimea yako kasha unamwagilia maji.

UMWAGILIAJI


Kuna haja ya kuhakikisha kuwa udongo unakuwa na unyevu mara baada ya kuotesha mbegu kama nilivyoeleza pale juu. Hii itafanywa kwa kuweka matandazo kwenye maeneo ambayo mbegu itakuwa imeoteshwa. Matandazo hayo yanapaswa kuwa makavu kwa sababu zifuatazo:-
 Mabichi huhifadhi wadudu.
 Matandazo mabichi husinyaa na kuachia nafasi.
Lakini pia unapaswa kumwagilia maji asubuhi na jioni mara baada ya kuotesha mbegu na kuweka matandazo huu ni msisitizo na juu nishaliongelea. lakini baada ya hapo inategemea na aina ya umwagiliaji unayotumia , pia ni vizuri kupima udongo ili ujue utamwagilia kwa muda gani na kila baada ya siku ngapi utarudia tena kumwagilia 

KUPAMBANA NA MAGUGU

Magugu hayapaswi kuwepo katika shamba kwani yakiwepo yatapambana na nafasi, mwanga, maji na virutubisho muhimu vipatikanavyo udongoni. Lakini pia kama magugu yasipoondolewa yatakuja kupunguza mavuno mwishoni. Hivyo basi napenda kushauri kuwa kama mkulima alime mara kwa mara kuondoa magugu kila yatapoonekana.

NB
Ni bora kama mkulima akaondoa magugu na mkono ili asije akaathiri mizizi ambayo ndo itakuja kutengeneza matunda.

MAGONJWA NA WADUDU

WADUDU

APHIDS
Wadudu hawa huwa na rangi tofauti tofauti mfano kuna ambao huwa na rangi ya dark brown na wengine huwa na rangi ya kijani (green), urefu wao huwa mm 2 na hupendelea kukaa chini ya majani na kufyonza tishu za mmea huko na wanapokuwa wengi hupelekea jani kujikunja na kusinyaa.

KINGA
Tafuta dawa iitwayo ATTAKAN C, ABAMECTING, DUDU ALL na nyinginezo za wadudu. Lakini pia kulima mazao ya mzunguko husaidia pia kupunguza wadudu hawa kwani itawafanya wasiyazoee mazingira ya shambani. Dawa hizi pia zitasaidia kuuwa wadudu wakatao majani.
MABAKA MEUSI
Huu ugonjwa huletwa na fangasi ambaye huingia katika majani na kusababisha mabaka. Mabaka haya huwa na kipenyo cha kuanzia mm 3 na huanza na rangi ya brown na baadae kuwa na rangi ya grey. Mara nyingine hutokea katika mauwa.

KINGA
 Kinga mbegu yako na madawa ukishaotesha mfano
Fanya kilimo cha mzunguko
 Epuka kutoamisha maji

UBWIRU CHINI (DOWNY MILDEW)
Dalili za ugonjwa huu ni pale ambapo jani litabadilika rangi na kuwa wa njano kisha baadae kuwa la brown kabisa. Lakini pia rangi ya grey yaweza kuonekana chini ya jani la mmea.

GAMBA LA JANI
Kwa maeneo ambayo udongo wao utakuwa na asidi nyingi. Majani huweza kuathirika na ugonjwa huu. Pale ambapo jani litetengeneza kitu kama gamba gumu hivi.

KINGA
Kinga ni kupima udongo kujua kiasi cha asidi kasha kupata ushauri juu ya hilo

KUTU YA MMEA
Hapa mmea huwa na vidoa vidogo vidogo sana ambavyo vina rangi ya machungwa au red brown.Ugonjwa huu mara nyingi hauna madhara makubwa kama mmea umeshaweka tunda.

KUOZA MZIZI NA KATA KIUNO (ROOT ROT AND DAMPING OFF)
Magonjwa haya hutokea sana katika maeneo yenye udongo mgumu unaokakamaa hasa udongo wa mfinyanzi. Hivyo hata mbegu uotaji wake huwa wa shida sana. Mbegu huanza kuota ikiwa na afya ambayo sio nzuri, mmea ukiwa mdogo waweza badilika rangi ukawa wa njano, ukasinyaa, kujikunja, mizizi kuwa na rangi nyeusi. Lakini pia kukata kiuno kwa mmea huweza tokea mmea ukiwa mdogo pale ambapo maji yatakuwa yakimwagiliwa bila kufuata mtiririko maalumu. Hii ikapelekea kutoamisha maji na hapo kupelekea mmea kujikunja na kuanguka.
KINGA
 Mbegu ioteshwe katika udongo mlaini uliotifuliwa vizuri
Inunuliwe mbegu kwa wauzaji wa kuaminika mara nyingi mbegu iwe inalindwa na thiram.
 Kufanya kilimo cha mzunguko
 Super grow au Mult k itumike kuongeza virutubisho kama boron kwa mmmea
 Mbegu isioteshe zaidi ya sm 2.5 kwenda chini
 Epuka kutoamisha maji na uwe na ratiba maalumu ya umwagiliaji.
Ingia hapam usome zaidi kuhusu magonjwa (http://www.shouragroup.com/v_Beet_e.htm)
MAVUNO
Kwa hecter moja mkulima anaweza kuvuna kati ya kilo 1000-1500,  na mmea huu huvunwa kwa mkono kwa kuvuta majani ya juu. Mbegu zinapatikana katika kampuni iitwayo RIGK ZWAAN arusha pande za USA RIVER, na kwa sasa wana branch hata bagamoyo. Kujua idadi ya mbegu anza na kuweka mashimo kwanza.
Picha: Beetrot zikiwa zimevunwa
KWA MAELEZO KAMILI:
(NA VITABU VINGINE VYA KILIMO NA MIFUGO)
+255 652 359 818
+255 767 359 818
a2mkono@yahoo.com
Green Agriculture is Your Farming friend 

Reactions:

1 comments:

Unknown said...

thanks alot, nimeanza kilimo hiki Mbeya na kinafanya vizuri
japo soko lake sijalijua vizuri, nimelima kwa majaribio

YouTube

GREEN HOUSE

GREEN HOUSE
BEST DESIGN

Visitors

LIKE US ON FACEBOOK

AGRICULTURE LAND

Mostly Visited